Mshindi wa tatu wa shindano la kuonja na kutambua radha ya bia za Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), ambalo liliwashirikisha baadhi waandishi wa habari Mkoa wa Mwanza, Emmanuel Chacha (kulia) wa ITV na Redio One, akipokea zawadi yake kwa furaha kutoka kwa Meneja wa kiwanda cha bia, TBL, Mwanza, Richmond Robert mwishoni mwa wiki.
Mwandishi wa habari wa Kampuni ya Business Times Ltd, Mwanza Jovin Mihambi akikabidhiwa zawadi ya ushindi wa pili na Meneja wa kiwanda cha bia (TBL ) Mwanza Richomnd Robert, katika shindano la kuonja na kutambua radha ya bia.
Waandishi wa habari Mkoa wa Mwanza, wakishindana kuonja na kutambua radha ya bia mwishponi mwa wiki katika Kiwanda cha Bia cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) cha Mwanza. Kutoka kulia ni Emmanuel Chacha wa ITV/ Redio One , Hellen Kabambo wa gazeti la Changamoto.
Waandishi walioshinda shindano la kuonja na kutambua radha ya bia wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa zawadi zao. Kutoka kushoto ni Meneja wa kiwanda cha Bia (TBL) Mwanza, Richomd Robert,, Jovin Mihambi wa Business Times, Jacquline Wanna wa gazeti la Kasi Mpya amnbaye alishika nafasi ya kwanza sawa na Henry Kavirondo , Emmanuel Chacha wa ITV na Redio One (katikatia), mshindi wa kwanza Henry Kavirondo wa Chanel Ten na Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa TBL, Editha Mushi.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Afisa Ubora wa Bia( TBL ) Jeremiah Kmammbi kuhusu bia inavyohifadhiwa .Waandishi walitembelea kiwanda hicho cha bia mwanza kabla ya kushiriki shindano la kuonja bia na kutambua radha ya aina ya bia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...