Rais wa Afrika ya Kusini,Mh. Jacob Zuma na Mai waifu wake mpya,Bi. Bongi Ngema wakikata jikeki wakati wa harusi yao iliyofanyika siku ya jumamosi KwaZulu-Natal nchini humo.
Rais Zuma na Mkewe Bongi Ngema Wakiwa na nyuso za furaha baada ya kufunga ndoa yao.
Rais Zuma na Mai Waifu wake wakiwa kwenye sherehe ya ndoa yao   kimila.
Rais Zuma akiwa amevaa ngozi ya chui na kubeba ngao wakati wa harusi ya kimila.
Kwaito kwa kwenda mbele wakati harusi ya kimila ikiendelea

RAIS wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, jana Jumamosi ameoa mke wa sita katika sherehe ya siku ya pili iliyopambwa kwa shamra za kabila la Wazulu. Rais huyo mwenye umri wa miaka 70 alimwoa Bongi Ngema siku ya Ijumaa katika mvumo wa nyimbo za Kizulu akiwa amevaa ngozi ya chui na kubeba ngao huku akiwa amezungukwa na wanaume waliokuwa wamvalia nguo za wapiganaji wa kijadi.


Msimamizi wa ndoa hiyo alikuwa ni mke wa nne wa Zuma aitwaye Nkandla katika sherehe iliyofanyika KwaZulu-Natal na kufuatiwa na sherehe za kisasa ambazo zilikuwa ni pamoja na kukata keki.

Zuma na Ngema wana mtoto wa miaka saba wa kiume. Ndoa hiyo ni ya tatu katika miaka minne iliyopita naya pili tangu ashike urais wa nchi hiyo mwaka 2009 akiwa rais mwenye wake wengi.

Kiongozi huyo ameoa mara sita na ana watoto 21 ambapo mmoja wa wake zake amekufa na mwingine ambaye ni Waziri wa Mambo ya Ndani, Nkosazana Dlamini-Zuma – ametalikiana naye. Wanawake hao hufaidika kwa kusafiri na rais huyo na kufanya kazi za ukatibu mahsusi, pamoja na kufuatana naye katika ziara za kiserikali.

Pamoja na kwamba Zuma aligharimia ndoa hiyo yeye mwenyewe, serikali pia imeongeza bajeti yake maradufu kwa zaidi ya Dola milioni mbili kutokana na kumwoa mwanamke huyo akiwa mmoja wa familia yake.

Hata hivyo, ndoa ya wanawake wengi inaonekana kupoteza umaarufu nchini Afrika Kusini ambapo ustaarabu wa nchi za Magharibi unazidi kuota mizizi ambapo idadi kubwa ya watu wa nchi hiyo hawakubaliani na utamaduni huo hivi sasa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Mama Mswati vile..Tofauti ni ndogo sana.Mswati anachukua wasichana wadogo ambao bado ni 'Bikra'......Kwa upande mwingine kudumisha mila nako ni muhimu..lakini suala la wake zaidi ya mmoja na dunia ya leo..Tafakari

    David V

    ReplyDelete
  2. mwassy ayoubApril 23, 2012

    Ni katibu Mukhtasi sio katibu mahsusi

    ReplyDelete
  3. This is to much, yaani hii ndio jinsi mwanamke anavyochukuliwa kama chombo cha starehe, hivi wanapima kweli?

    ReplyDelete
  4. Marais wa kiafrica hicho ndicho wanaweza,sijui kuna legacy gani ameacha ktk muda wake wote tangu awe rais,zaidi ya kuoa,shame on him.

    ReplyDelete
  5. Mke wa sita, watoto 21 anao tayari, ni kipi kipya anachotafuta kama sio kuongeza tu gharama kwa nchi yake?

    ReplyDelete
  6. Wadau hii imekaaje? raisi wa Nchi ana majukumu mazito sana, sasa hapa wake 6 inakuwaje? na umri huo mke wa sita wa nini? Jee kama kiongozi wa Nchi kubwa kama SA kuoa wake wengi kiasi hiki ninini anawafundisha raia wake katika Dunia ya leo? SIPATI JIBU MIE NAONA NI UKICHAA FULANI HIVI.

    ReplyDelete
  7. Aaah dume la mbegu weee,kama kawaida yako!

    ReplyDelete
  8. harusi ya kimila ila prezidaa kapiga raba mtoni

    ReplyDelete
  9. This is utterly SELFISHNESS!

    ReplyDelete
  10. Ndio mila za kiafrika, na hao wenzetu bora wanahalilisha kuvuta jiko. Kuliko wanaume wengi wa kiafrika kuwa na nyumba ndogo kibao zisizo halali.

    Na hujo ughaibuni maraisi wao kutwa skendo za kulala nakina dada poa au kubaka. Ss si bora uhalalishe kuliko kutwa kupiga kila sehemu kama wanyama.

    ReplyDelete
  11. Naona ndugu zangu bado mnatawaliwa kifikra. Je, kwa nini tuachane na mila zetu na tufuate mila za nchi za magharibi? Kuoa wake wengi ni mila na desturi za kiafrika. Sasa Zuma anadumisha mila. Big up Zuma. Waoneshe watu umuhimu wa mila zetu.

    ReplyDelete
  12. Mdau wa maguApril 23, 2012

    Wanaumeeeee eeeeeh.Huo ndio uafrika halisi.mambo kadesadesa hamna.penda sana hii move ya zuma. Kiliko kijificha vimada zaidi ya kumi tunaona hawa viongozi wetu. Unalaumiwa kwa kuwa muwazi,fanya open mwan wane... wanaumeeee eeeeh

    ReplyDelete
  13. Katerero tu hapo hamna kitu

    ReplyDelete
  14. Huku kuoa sana sio kigezo cha kuwa 'Kijogoo'

    Umri wake umekwenda na pumzi zimeshashuka sasa huu si imebaki ubishi tu?

    Cha zaidi anatafuta kuweka Rekodi kwa Raisi wa Kwanza Duniani kufia kifuani mwa mwanamke!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...