Na Mwandishi wetu

Kocha mpya wa Yanga, Marcio Maximo anatarajiwa kuwasili nchini wiki ijayo kwa ajili ay kuinoa timu hiyo kwa ajili ya mashindano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati maarufu kwa jina la Kagame cup.

Kocha huyo atawasili nchini pamoja na kocha msaidizi wa viungo. Pia katika msafara huo atakuwepo mke wake kutokana na ukweli kuwa Maximo hatakuwa na mpango wa kurejea kwao mpaka kumalizika kwa michuano ya Kagame.

Chanzo kutoka klabu ya Yanga kimesema kuwa Maximo amekubaliana na Yanga kwa ajili ya kuinoa timu hiyo na tayaria ametoa mapendekezo kadhaa ya usajili wa wachezaji kwa ajili ya msimu ujao.

Mapendekezo hayo ni pamoja na usajili wa wachezaji kadhaa kwa ajili ya kikosi chake na tayari klabu hiyo imekwisha kamilisha kwa asilimia kubwa. Wachezaji hao ni pamoja na kipa Ali Mustapha ‘Barthez’ na beki wa kati wa Simba, Kelvin Yondani ambaye amezua gumzo kubwa hapa jijini.

Mtoa habari amesema kuwa Barthez amekwisha saini mkataba wa klabu hiyo huku Yanga ikimtoa kwa mkopo kipa wake, Shaaban Kado kurejea timu yake ya zamani ya Mtibwa Sugar.

Wachezaji wengine nyota waliosajiliwa na klabu hiyo kwa ajili ya msimu ujao ni beki wa timu ya Kagera Sugar, David Luhende, Mussa Hassan Mgosi kutoka timu ya DC Motema Pembe, Owen Kasule kutoka klabu ya Hoàng Anh Gia Lai Football Club ya Vietnam ambaye ni raia wa Uganda, Meddie Kagere (Polisi, Rwanda), Nizar Khalfan na Kelvin Yondani. Pia wamo akina Saidi Bahanuzi na Juma Abdul kutoka timu ya Mtibwa Sugar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 08, 2012

    Itakua poa sana kwani Mzee Marcio Maximo anajua sana huyo ataifikisha mbali timu YAnga pia kuzijua kwake vizuri timu za Bongo kutamsaidia sana kwani anazijua changamoto la soka letu A 2 Z

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 08, 2012

    Ama kweli Manji a.k.a Sheikh Mansoor ameamua kuua mwaka huu, sijui kama atapona mtu mpaka Maximo ndani.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 08, 2012

    Hajui fitina za mpira wa bongo huyu

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 08, 2012

    Swadatah!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 08, 2012

    Tanzania kuna hela na ukiwa mwajiriwa mgeni unaweza kutajirika haraka sana Bongo.Attention anayopata Maximo huko bongo kamwe hawezipata kwao Brazil.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 09, 2012

    Hata wabongo wanapata attention, hata kama ni kudharauliwa!

    sesophy

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 09, 2012

    Nawashangaa sana wabongo wanaomuona Maximo ni kocha wa maana, mi namuona ni mbabaishaji tu, anapenda TZ kwa kuwa kuna watu hawajui kocha wa maana ni yupi. Kama atakaa sana Yanga iko siku watakuja kumtoa kwa bakora

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 09, 2012

    nafikiri huu ndo utakuwa mwisho wa ye kuipenda Tanzania mwache aje kukopwa

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 09, 2012

    LAzima SImba apakatwe mwaka huno !!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...