Kwanza natoa pongezi kwa blog ya jamii Issa Michuzi kwa kutupa nafasi ya kujadili mambo mazito kama haya.
Jibu
Hoja nzuri.Ila ...
 
Siyo watanzania wote waishio nje ya nchi wamebanwa na maisha.
Wako matajiri wako wakawaida n.k sidhani kama kuna mtanzania maskini hapa ninapoishi ila kama yupo kwa nini tusimsaidie?

Watanzania wengi wanaipenda nchi yao ila kunakubaguwana kimtindo ndiyo maana wengine wanaamuwa kuacha kabisa kuzungumzia maswala ya nyumbani (Tanzania) kwa sababu inakuwa kama tunazungumzia maumivu tu kila siku.
 
Mimi nimeshakutana na mtu ana-miaka zaidi ya 40 Ulaya na kwa bahati nzuri mke wake anataka waje nyumbani kutembea na Mtanzania anakataa.Tatizo si kuwa wao ni maskini wanaingiza zaidi ya milioni kumi ya kitanzania kwa mwezi.

Tunapozungumzia kurudi Tanzania ?
Wazungu wanaita (Maswala ya energy thief)Maana yake unamkuta mtu ametulia na familia yake vizurii(wanakula bata :) alafu unaanza kumkumbusha mambo ya Huzuni ni kama vile unamuibia furaha yake.

Ila kuna wengine wanakutana matatizo fulani ya kiubaguzi, haswa nchi za Ulaya. Wao wanakuja kwentu kwa raha na inabidi watu wetu waishi kwa raha ,baadhi ya wazungu wameanza kulielewa hili na mda si mrefu litakuwa si tatizo tena.Mtanzania ana haki ya kuheshimika kwa sheria za Umoja wa Mataifa iwe ameunja sheria au la cha msingingi ni yeye kujuwa haki yake.

Mtanzania hana aja ya kubaguliwa  kwa sababu Tanzania tumesaidia wakimbizi wengi tunakaribisha mtu wa kila aina lakini tunapokuwa nje ya nchi tunanyanyaswa mwanzo kwa sababu tunakadamu fulani wenyewe wanaamini kadamu cha akili :)kwa hiyo huwa Mtanzania wa kawaida inabidi wakupe  mda fulani kama miaka 4 hivi ya kufundishwa ubababiloni alafu unafanikiwa . Hii si haki, kunawatu wa Afrika magharibi na nchi nyingine wanakubalika hata kama wameingia kwa njia za mkato.

Sisi watoto wa Jakaya tumeamuwa tutakuwa tunarudi nyumbani na kuakikisha tunaitangaza nchi tunatangaza kweli ya Mtanzania ni nini (mfano tunapinga uharibifu wa mazingira na tutapigania hili mpaka vizazi vijavyo.
 
alafu tunaadopt maendeleo mazuri ya huku  ili kuiletea nchi mafanikio zaidi.Hii imetokana na mtazamoa wa mtanzania wa sasa ni tofauti na ule wa Zamani.Watanzania wengi wameelimika pia mtazamo wa Dunia kwa sasa umebadilika Wageni wengi wataamia nchi za Afrika.
 
Nchi nyingi za Afrika zitafanikiwa  baada ya mika 15 ijayo.
Na uthibitisho wa baadhi ya Wazungu waliofanya safari za utalii huko ambao wanaamini nchi  ya Tanzania inaendelea kwa kasi imebakia kitu kidogo tu  kurekebisha baadhi ya sheria za kuishi kwenye Usasa ambazo ndizo tunaishi sasa.Hauwezi kujenga nyumba ya ghorofa ya cement na msingi uwe wa Udongo mbichi tena wenye mchanga kidogo the the :=)
 
Kuna haja ya kutoa elimu zaidi ya haki ya mtu na ni jinsi gani ataamini anaitetea haki yake kwenye njia sahihi.
 
Cha kufanya
1.Tuwatambue Watanzania wote waishio nje ya nchi na washirikishwe na kupewa heshma ya Utanzania kwa sababu wao   ndiyo mabaloozi wa nchi yao ugenini.Tukifanya hivi watanzania waishio nje wanaweza kuwadhamini acomodation wanachuo wengi kuja kusoma nje ya nchi.mafano Ethiopia wameleta wanachuo wengi mwaka jana hapa ninapoishi.Wanawenyeji wanaowadhamini chakula na elimu ni bure.

2.Kuweka sheria kali za Rushwaili angalau kuwe na adabu fulani mtu anapofikiria kupokea rushwa.

3.Kuwa na uhuru wa kuongea hili tunalifanyia kazi vizuri ,inabidi tuwapongeze watu wa blogs pamoja na Serikali ya sasa Raisi ,mzee mzima Nape baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa n.k kwa kuwekea mkazo hili(Heshma si hofu,hofu kwenye heshma  ni unafki)
 
4.Tuwe na lishe ya kawaida ambayo kila mtanzania anaweza kununuwa kwa siku.
Nchi za Magharibi zilianzisha vitu kama MC Dolnad ila sisi tuongeze wawekezaji wazalendo kwa kuiga mfano wa Jiko la Shoprite.
Wabunifu wabuni ni jinsi gani muuza miogo au chipsi anaweza kuwa na duka la kisasa la kuuzia bidhaa zake.

Nakumbuka tuna sehemu wanaziita za mamalishe kwa huku ulaya wametengeneza Hall lenye majiko Mengi ya kisasa na wameweka vyakula vya nchi maarufu kama vile India n.k

Wauzaji wanalipa kodi kwa mwekezaji ambaye anaweza kuwa ni mtu binafsi au serikali.

Mwekezaji anapaswa kuangalia sehemu inafanyiwa kazi ni salama pamoja na mbambo mengine.

Kila mtanzania awe mlinzi wa mali za nchi azielewe vizuri sheria n.k
Tujenge utaratibu wa kuwapongeza viongozi wanaofanya vizuri.kuwafanya wawe mfano kuwatangaza kwenye lugha zote na wajisikie kuwa wao ndiyo mashujaa wetu.
Tanzania tunanguvu sana,ndiyo maana inakuwa vigumu kushirikiana.

Tunawatu kilapande ya Dunia.
Tuna mtu katika kila lugha inayozungumzwa Duniani sidhani raia wa Uingereza wanawawakilishi katika lugha nyingi kama sisi watanzania.
Naomba radhi kama nitakuwa nimeandika kiswahili finyu :) nadhani mtalielewa lengo langu.
 
Mdau

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 23, 2012

    I think this is a good discussion.
    Nimgependa kuchangia kw akusema kuwa ni kweli kuwa huku tulipo kuna watu wameshindwa na maisha na wengine wameyamudu.Ila kila mtu likuja na njia yake na kujumlisha kila mtu pamoja inatia dosari.
    1. Kudai kuwa nyumbani ni Tanzania nadhani ni sawa ila nyumbani kwa mtu ni pale alipo na familia yake. Wengi tunazungumzia nyumbani tukimaanisha Dar es salaam. Ila wengi sio wa Dar kwetu ni Gezaulole, ila Dar ni kweru maana tumejenga huko na Gezaulole tunakwenda kusalimia. Kutokana na technologia iliyopo ninaweza kuongea na ndugu hakta kwa kuonana uso kwa uso wakati wao weinyewe hawazewi kuonana hata Dar na Kigoma.Ninaweza kuhudhuria shuhuli yoyote hapo toka huku Marekani kabla hata aliyeko Mwanza hajafika Dar.
    Mamabo yanayotufanya tuishi huku ni kuwa unapokuwa na watoto ambao Mungu kawasaidia kusoma elimu hii ambayo watoto wa mawaziri waliisoma Basi itakuwa ni kama laana kuwarudisha kuja kuhangaika na elimu ya kufuta ujinga na shida zingine amabazo Mungu kawaipushia.
    Kama nikifa leo nitapenda kuzikwa hapa ambapo watoto wangu watatembelea kabuti langu maana ndugu ni nani hasa ila mke na watoto?
    Nilikuwa Tanzania 2008 na nikapenda kuweka IT company mizengwe niliyopitia kupata lesi=eni ilikuwa miubwa. Mimi sikusomeshwa na Serikali hapa US nilijipiga mwenyewe, sasa iweje nisome na niwaletee maendeleo kisha mninyanyase wakati Waamerica ukishasoma wanapenda kukubakiza hapa?
    Mentalite ya Viongozi ni mbaya zaidi, taanzania haiongozwi na wenye sifa, inaongozwa na wajanja wajanja. Tulipobadilisha pasport hapa US afisa ubalozi mmoja wa Tanzania alitukalisha siku mbili tukisubiri kwenye foleni ili tujaze form. Nilipofikiwa nilimuliza kama wangependa tuwatengenezee form za kujazo online na watu waje wameshajaza iwe ni zoezo=i la kuchukuwa fingerprints. Jibu lake lilikuwa hivi. "Sasa kijana ukifanya hivyo sisi tutakula wapi?'Ninaamini shida ya Tanzania sio rasilimali ila ni asili yetu. Hata huku tuliko Wanaijgeria, wakenya wanatuajizi sisi ni watu wa mdomo.
    Mungu ibariki Tanzania

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 23, 2012

    Nafikiri wengi wenu hamkumuelewa aliyeanzisha hii mada. Mwenyewe hakusema watu warudi nyumbani ila alisema watu wanaona aibu kurudi nyumbani kwa sababu wamepigika. Jambo ambalo ni kweli. Wapo ambao wangependa kurudi lakini wakashindwa kwa sababu hizo. Wanaona aibu.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 23, 2012

    KURUDI TANZANIA NI KAMA KIFO KIMEKUTOKEA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...