Bwana Alex Mwaipasi katibu Mkuu wa chama cha kuogelea akizungumzia maonyesho yatakayokuwa maalum kwa ajili ya kutoa elimu ya jinsi ya kutumia maji wakiwa salama ikiwa ni pamoja na kujua jinsi ya kujiokoa unapopata dharura ya kuzama kwenye maji kushoto ni John Belele Mwenyekiti wa chama cha kuogelea, Maonyesho hayo yatafanyika kwenye viwanja vya Tanganyika International School Upanga jijini Dar es salaam kuanzia Juni 27-29

Tanzania Life Saving Society (TALISS) ni taasisi ya kitaifa isiyo ya kiserikali ambayo jukumu lake kubwa ni kuzuia/kupunguza idadi ya vifo vinavyosababishwa na maji, kwa njia ya kutoa elimu kwa jamii jinsi ya kuishi salama karibu/ndani ya maji, pamoja na kusimamia maswala ya usalama kwa watumiaji wa maji ya wazi (Open water) na mabwawa (Swimming pools).

Katika kuendelea kutimiza wajibu wa kuelimisha jamii, Tanzania Life Saving Society (TALISS), kwa mara ya kwanza inazindua Wiki ya Kuzuia Vifo Katika Maji Kitaifa (NATIONAL DROWNING PREVENTION WEEK) utakaofanyika katika shule ya kimataifa ya Tanganyika (IST) iliyopo upanga Dar es salaam, kuanzia tarehe 26 mpaka tarehe 30 Juni, 2012 kila siku saa 8:00 mchana mpaka saa 11:00 jioni, sambamba na hilo TALISS pia itakuwa inaadhimisha miaka 20 ya kuzaliwa kwake.

Katika uzinduzi huo tutatoa semina na kufanya maonesho mbalimbali, ambapo kusudi kuu la tukio hilo ni kukuza na kueneza elimu ya uokoaji na usalama katika maji hapa nchini.

Tunatanguliza shukrani zetu za dhati kwa ushirikiano wenu.
Wako katika uokoaji wa maisha,

ALEXANDER H. MWAIPASI
KATIBU MKUU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...