Habari za kusikitisha zilizotua katika mtandao  wa www.francisgodwin.blogspot.com asubuhi hii kutoka mkoani Morogoro zinaeleza kuwa aliyekuwa mhariri wa habari wa gazeti la Jamboleo Willy Edward (pichani) amefariki dunia .

Willy Edward alikuwepo mkoani Morogoro katika mafunzo ya siku moja pamoja na wanahabari wengine na kuwa inadaiwa alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa pumu kwa muda mrefu .

akithibitisha juu ya taarifa hiyo mhariri wa habari wa gazeti la Mtanzania Kulwa Karedia ambaye walikuwa wote na Willy mjini Morogoro amesema kuwa hadi majira ya saa 3 usiku walikuwa wote na baada ya hapo aliwaaga wanahabari wenzake kuwa anakwenda kulala .

Kwa upande wake mpasha taarifa wa kwanza kabisa katika mtandao huu Dotto Mwaibale aliueleza mtandao huu kwa njia ya siku kwa kutumia maneno wachache sana kuwa mzee wa matukio umepata taarifa kuwa Willy Edward Amefariki Morogoro?

Huku kwa upande wake katibu wa jukwaa la Wahariri nchini Nevelin Meena akieleza kusikitishwa na kifo cha mhariri mwenzao huyo na kuwa amepokea kwa masikitiko makubwa juu ya kifo hicho.


Mtandao huu jana majira ya saa 11 jioni ulipata kuzungumza na Willy Edward kwa mara ya mwisho kwa njia ya simu ambapo alitaka kujua zaidi juu ya kile alichozungumza katibu wa itikadi na uenezi wa CCM Taifa Nape Nauye akiwa ziarani wilayani Kilolo ili habari hiyo kuwasiliana na ofisi yake wapate kuitumia katika gazeti la Jamboleo la Leo ,habari ambayo imetumika ikiwa na kichwa cha habari Nape awaonya makandarasi Kilolo .
Nukuu ya willy Edward jana katika mazungumzo yetu kwenye Simu 

Mzee wa matukio daima Mambo vipi ?
nimesoma katika mtandao wako juu ya ziara ya Nape Kilolo sasa nitampigia simu mhariri wa habari jumapili Said Mwishehe ama Beny Kisaka ili aweze kuitumia habari hiyo kwani nimeipenda sana jinsi ambavyo Nape alivyogeuka mwimba kwa kupigania ajira za vijana ...mimi nipo Morogoro katika semina mara moja kesho nitageuza Dar ... wasalimia rafiki zangu Salim Asas na Daud Yassin muulize pia Yassin vipi mwaka huu kombe la Muungano Mufindi alicheka Ha! Ha! Ha! na kukata simu

mpenzi mdau wa mtandao huu habari zaidi juu ya kifo cha Willy Edward utaendelea kuzipata zaidi katika mtandao wa endelevu wa Iringa wa www.francisgodwin.blogspot.com

Sote tulimpenda sana Willy Edward ila Mungu kampenda zaidi yetu hivyo jina lake Mungu na lihimidiwe zaidi .

Amina

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 17, 2012

    Willy, ulikuwa mtu mzuri na mkarim sana .Nimehuzunishwa mno na hii taarifa ya kushtua .May God rest your soul in peace .We shall miss you, but we shall never forget you.
    Sauda Simba

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 17, 2012

    Mungu ailaze mahala pema Roho ya marehemu Willy, alikuwa mcheshi na mkarimu mwenye furaha muda wote. RIP

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...