Bw. Onesmo Ngowi akiwa na mcheza sinema 
maarufu wa Marekani Deidre Lorenz
Baada ya mafanikio makubwa ya kumleta mcheza sinema maarufu wa Marekani Deidre Lorenz kushiriki mbio za Mount Kilimanjaro Marathon zilizotimua vumbi tarehe 24 Juni 2012 sasa klabu ya Mout Kilimanjaro Marathon 1991 imeanzisha mbio za “Great Kilimanjaro Run – GKR”

GKR zitafanyika mjini Moshi kila mwaka kuanzia tarehe 22 - 28 October 2012 zikishirikisha klabu zote za riadha kutoka mkoa wa Kili manjaro. GKR itazishikisha mbio fupi (Track and Field events) na kumalizia na marathon siku ya jumapili tarehe 28 October.

Akizungunzia uamuzi wa kushirikisha mbio fupi katika GKR Rais wa klabu ya Mt. Kilimanbjaro Marathon 1991 Onesmo Ngowi alisema kuwa klabu yake inataka kuziendeleza pia mbio fupi na michezo mingine ya uwanjani badala ya kuweka juhudi zote kwenye marathon tu.“Watu wamekazania sana marathon na kusahau mbio fupi ambazo zilishawahi kuliletea taifa hili sfa kubwa sana” alisema Ngowi kwa msisitizo.

Kuanzishwa kwa GKR kutaufanya mji wa Moshi kuwa na mbio tatu za marathon kwa sasa na hii inaufanya mji huu kutoa nafasi kubwa kwa wanariadha kukuza na kuendeleza vipaji vyao.

Tutamleta Haile Gabreselasie aje kuzindua mbio hizi” alisema Ngowi ambaye mwaka jana alikuwa na mazungumzo marefu jijini Addis Ababa na gwiji hili la mbio ndefu duniani kutoka nchi ya Ethiopia. Ngoiwi aliweza pia kutiliana mkataba na shirika la ndege la Ethiopia (Ethiopia Airlines) jijini Addis Ababa kufadhili mbio za Mount Kilimanjaro Marathon. Kwa sasa Ethiopia Airlines (ET) ndio wafadhali pekee wa Mount Kilimanjaro Marathon. ET wanatoa punguzo kwa wakimbiaji wanaoshirtiki kwenye mbio hizi kutoka sehemu mbalimbai duniani.

Aidha, ET wanalipia gharama za kutangaza mbio hizi wakati wa New York Marathon, L.A Marathon na Boston Marathon. Hii inaitangaza sana Tanzania kwani mbio hizi tatu zinawashirikisha wakimbiaji wengi sana kutoka katika nchi nyingi duniani. Kwenye mbio hizi za Marakani Mt. Kilimanjaro Marathon huweka banda la maonyesho linaloitangaza Tanzania na vivutio vyake.

Pia Mt. Kilimanjaro Marathom huchezesha nahati nasibu (raffle) kwenye mbio hizi tatu za Marekani ili kuwapata washiriki maarufu kama Deidre Lorenz kuja kukimbia na kuitangaza vyema Tanzania.

Aliendelea kusema kuwa nchi hii ni yetu sote hivyo tuna jukumu la kuitangaza na kuiendeleza wote alisisitiza Ngowi ambaye mwaka 2000 ofisi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilimpa tuzo ya “Mwanateknolojia wa Karne ya 20” kwa juhudi zake za kuendeleza Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).

Ngowi anawaalika watu binafsi, makampuni na taasisi kushirikiana naye kuendeleza Utalii wa michezo hapa Tanzania ili kuipeleka nchi hii hatua moja mbele kwenye utandawazi. Kwa wale wanaotaka kuwasiliana naye kuhusu ufadhili watumie anwani ya barua pepe yangowio@yahoo.com au wapige simu namba 0754-360828.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 28, 2012

    Mzee mwenye shati la KITENGE mbona wambana mwenzio hivyo?...LOL!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...