Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Rais Somalia Mheshimiwa Sheikh Shariff Sheikh Ahmed leo Juni 4, 2012 kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro, baada ya mgeni huyo kuhitimisha ziara yake ya siku mbili nchini. Rais huyo wa Somalia alikuja nchini kwa mazungumzo na Mheshimiwa Rais Kikwete ambapo alitoa shukurani zake kwa Tanzania kutokana na misaada mbalimbali ya kibinadamu iliyopata na inayoendelea kupata pamoja na kuisemea vyema Somalia katika medani za Kimataifa na za Kikanda kila alipopata nafasi hiyo. PICHA NA IKULU.

Rais wa Somalia Mheshimiwa Sheikh Shariff Sheikh Ahmed leo, Jumatatu, Juni 4, 2012, ameondoka nchini kurejea nyumbani baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini. Rais Ahmed aliwasili nchini Jumamosi, Juni 2, 2012.

Kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) Rais Ahmed ameagwa na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.

Rais huyo wa Somalia alikuja nchini kwa mazungumzo na Mheshimiwa Rais Kikwete kuhusu hali ya kisiasa na kiusalama nchini mwake na ameishukuru Tanzania kutokana na misaada mbalimbali ya kibinadamu ambayo imekuwa inatolewa kwa nchi yake.

Rais Sheikh Ahmed pia amemshukuru Rais Kikwete kwa kuisemea vyema Somalia katika medani za Kimataifa na za Kikanda kila alipopata nafasi hiyo.

Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, kesho Juni 5, 2012 anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, itakayoadhimishwa kitaifa mjini Moshi.

Imetolewana:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
DAR ES SALAAM.

04 Juni, 2012

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 06, 2012

    Assalam Alaykum,

    Raisi wa Somalia Sheikh Sharrif kama unavyomuona Raisi wetu Mhe.JK bado ni handsome man na sisi Wananchi ni hivyo hivyo na zaidi ya hapo nchi yetu ina watu wa Dini zote na tunaheshimiana vizuri tu!.

    Hivyo fanya mpango wa Kitaifa Utuletee Wanawake wa Kisomali wa kuoa na tuongeze undugu na Ushirikiano zaidi!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...