Na Juma Mohammed,MAELEZO Zanzibar

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imesema imedhamiria kwa dhati kupambana na madawa ya kulevya nchini na kuwaomba wananchi wasaidie juhudi hizo.

Hayo yameelezwa jana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Fatma Abdul-habib Ferej alipokuwa akijibu msuali ya wajumbe wa baraza la wawakilishi huko Chukwani Mjini Zanzibar.

Awali katika suali la msingi la Mwakilishi wa nafasi za wanawake (CCM) Panya Ali Abdallah alisema miaka sita tangu washirika wa maendeleo UNDP kutoa msaada wa choo cha flashi cha madawa ya kulevya ambacho kilitegemewa kufungwa katika uwanja wa ndege na kuhoji ni sababu zipi zilizopelekea choo hicho kutofungwa hadi sasa.

Akijibu suali hilo Waziri Fatma alisema alisema sababu za kuchelewa kufungwa choo hicho ni pamoja na kutopatiwa kwa eneo muwafaka mapema kwa mamlaka husika kwa ajili ya kujenga choo hicho hasa kwa kuzingatia mazingira ya eneo husika.

Aliwaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi kwamba msukumo mkubwa wa hatua iliyofikiwa sasa ilichangiwa kwa kiasi kikubwa na mwenyekiti wa tume kwa wakati huo.

“Napenda kumjulisha mheshimiwa mjumbe kwamba choo hicho sasa kiemshafungwa, yaliobaki ni mambo madogo madogo tu ya kumalizia ili kianze kutumika” alisema Waziri huyo.

Akijibu suali la mwakilishi huyo kwamba haoni kama kuchelewa kutoa huduma kwa choo hicho kutaweza kuwavunja moyo washirika wa maendeleo, kitendo hicho cha kuchelewa kinaweza kutafsiriwa hivyo.

“Napenda kuungana na mjumbe katika hilo kuwa kitendo chetu cha kuchelewa kinaweza kutafsiriwa na washirika wa maendeoe kuwa ni kuwavunja moyo katika mapambano dhdii ya ya madawa ya kulevya” alisema.

Hata hivyo alisema nia na lengo la serikali kwa ujumla katika vita dhdii ya dawa za kulevya ni thabiti na ila lengo la kuona kwamba inatumia zahudi zake zote katika kukabiliana na janga la madawa ya kulevya.

Waziri Fatma alisema usalama wa uwanja wa ndege ni muhimu kwa wageni na weneywe na serikali inaendelea na juhudi za kupambana na waletaji na wasafirishaji wa madawa hayo.

Akijibu suala la kukosekana kwa choo hicho kunazorotesha juhudi za mapambano dhidi ya madawa ya kulevya, Waziri alisema kutokuwepo kwa choo katika uwanja bado hakujaathiri shughuli za kupambana na madawa ya kulevya.

“Kwa kweli naomba niseme kwamba kukosekana kwa choo hakujaathiri hata kidogo vita dhidi ya madawa ya kulevya kwa sababu wanaohusika wanawachukua watuhumiwa na kuwapeleka katika hospitali ya mnazi mmoja na kazi hizo hufanywa huko”alisema Waziri huyo.

Aidha alitoa wito kwa taasisi za dola zilizopewa majukumu ya udhibiti kuunga mkono juhudi za serikali na washirika wa maendeleo katika kukabiliana na janga hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...