Taifa Stars imetolewa kwenye mechi za mchujo za Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kufungwa kwa penalti na wenyeji Msumbiji (The Mambas) katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Taifa ulioko Zimpeto pembeni kidogo ya Jiji la Maputo.

Refa Bennett Daniel alipopuliza filimbi ya kumaliza dakika 90 za pambano hilo timu hizo zilikuwa zimefungana bao 1-1, hivyo kwa mujibu wa kanuni za mashindano hayo yanayoandaliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) mikwaju ya penalti ikatumika kupata mshindi.

Katika mechi ya kwanza iliyochezwa Dar es Salaam, Februari 29 mwaka huu timu hizo 
zilitoka sare ya bao 1-1.


Msumbiji ndiyo walioanza kupata bao dakika ya 9 lililofungwa na mshambuliaji Jeremias Sitoe akiungnisha krosi ya Elias Pelembe ambaye mabeki wa Taifa Stars walifikiri ameotea.

Stars ilisawazisha bao hilo dakika ya 89 likifungwa kwa kichwa na
Aggrey Morris kutokana na mpira wa kona uliopigwa Amir Maftah.
Mikwaju ya penalti tano tano walioifungia Stars walikuwa Amir Maftah, Shabani Nditi na Shomari Kapombe wakati Aggrey Morris na Kevin Yondani.
Kwa vile The Mambas nao walikosa mbili ikabidi iongezwe penalti moja moja. Waliofunga kwa upande wa Stars walikuwa John Bocco, Frank Domayo na Mrisho Ngassa wakati Mbwana Samata alikosa.

Akizungumzia pambano hilo, Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen aliwapongeza wachezaji wake kwa kupambana hadi dakika ya mwisho.
"Tulikuja Maputo tukijua kuwa tunatakiwa kufunga bao, tumeweza kufunga bao ingawa katika dakika za mwisho. Unajua linapokuwa suala la penalti chochote kinaweza kutokea, na ndivyo ilivyokuwa," alisema Kim.

Taifa Stars itarejea nyumbani Juni 19 mwaka huu, ambapo itaaondoka hapa saa 4.40 asubuhi kwa kupitia Nairobi, Kenya na kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 1.50 usiku.

Kikosi kilipngwa hivi; Juma Kaseja, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni/John Bocco, Aggrey Morris, Kevin Yondani, Shaabani Nditi, Mrisho Ngasa, Frank Domayo, Thomas Ulimwengu/Haruna Moshi, Mbwana Samata na Mwinyi Kazimoto/Amir Maftah.



Boniface Wambura
Ofisa Habari 
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 17, 2012

    Safi sana vijana.Matatizo ya kutolewa yameletwa na Kocha aliyetoka Jan Poulseni aliyeruhusu sare ya 1-1 nyumbani.Wambura timu isivunjwe hii.Tumepata kocha,tumepata timu..Hizi mechi ziwe za kuijenga timu.Akili ziwe kuifunga Morocco March 2012.

    David V

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 17, 2012

    hehehe, tukubali u soka sio mchezo wetu tuingie kwenye kurusha nchale, mkuki na kukimbia na wale waliozungukwa na maji waingie kwenye kuogelea na rowing!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 18, 2012

    Wapi air Tanzania watani wa jadi bado tu wanatupiga mabao, msumbiji ipo chini yetu lakini leo hii unaruka hadi kenya then unarudi tena Tanzania. anyway 1-1 ilikuwa sio mbaya sana.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 18, 2012

    Pole zenu, elekezeni nguvu zote katika ufisadi huko mnaweza kutwaa taji la dunia.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 18, 2012

    Punda ndo yule yule anabadilishwa soji tu kila siku. kama punda mzee mzee tu ata umfanye nini na akigoma ujue kagoma ata umuue haendi. Lini hawa watu watafahamu?

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 18, 2012

    Mheshimiwa sana kaka yangu Leodgar Tenga nakukumbuka sana ukiwa kibaha na ndogo wako Sendeu tulikuwa nae pale Mwakangha St Francis College (Pugu)akitokea Kikimbo kule Ilonga na nakujua kuwa wewe ni fundi(Engineer mahiri sana)Kaka, Hili la uongozi wa Soka naona linataka kukuchafulia kidogo! Kaka si uondoke tu kwani ni mpaka wakufungie nje!Kina dada out! Kaka zao out! Juzijuzi simba na out! Naogopa kusema Kagame ijayo itakuwaje labda klabu inayolitetea kombe lenyewe klabu yako ile ya zamani wataweza kulizuia baada ya mitifuano na mchunga!Ila brother let us be serious likitoka na hilo just call a press conference and tell theo enough is enough im quitting TFF

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 18, 2012

    Kazi nzuri Taifa Stars mmepambana ndivyo inavyotakiwa

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 18, 2012

    Hata msumbiji? Hongereni kwa kutolewa!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...