Mchezaji wa timu ya soka ya NBC,  Ibrahim  Makoye (kulia) akimiliki mpira mbele ya Khatibu Shilumba wa timu ya Barclays katika mchezo wa kirafiki  uliofanyika katika Viwanja vya TCC Club, Chang’ombe, Dar es Salaam leo. NBC ilishinda kwa penalti 4-3.
 Mkurugenzi wa Technolojia Habari wa Barclays, Dakshit Pandya (katikati) akikabidhi kikombe cha ushindi wa kwanza kwa nahodha wa timu ya soka ya Benki ya NBC baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-3 katika mchezo wao wa kirafiki uliofanyika jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Technolojia Habari (IT) wa NBC, Pete Novat.
 Mkuu wa Idara ya Teknolojia Habari (IT)  wa Benki ya NBC,  Pete Novat(kulia) akikabidhi kikombe cha ushindi wa pili kwa nahodha wa timu ya soka ya Barclays, Siaga Mgweno mara baada ya mechi ya kirafiki baina ya timu za benki hizo iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. NBC ilishinda kwa penalti 4-3. Katikati ni Mkurugenzi wa IT wa Barclays, Dakshit Pandya.
Wachezaji wa timu ya soka ya NBC wakishangilia baada ya kuibuka kidedea kwa kuinyuka timu ya Barclays kwa mabao 4-3 katika mchezo wa soka wa kirafiki jijini Dar es Salaam mwishoni leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...