Mussa Twangilo ambaye ni mhariri kutoka TBC Taifa akiuliza swali wakati wa mkutano wa wahariri na waandishi wa habari waandamizi kuhusu sensa ya watu na makazi iliyotarajiwa kufanyika tarehe 26 Mwezi wa nane mwaka huu. Mada mbalimbali zilijadiliwa katika mkutano huo wa siku moja ulifanyika jana mjini Morogoro.
Afisa Uhamasishaji sensa ya watu na Makazi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Said Amir akiwaonyesha wahariri na waandishi wa habari waandamizi (hawapo pichani) kitabu cha ufafanuzi wa maswali ya sensa ya watu na makazi mwaka 2012. Wanahabari hao walihudhuria mkutano wa siku moja wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 ulioandaliwa na ofisi ya Taifa ya Takwimu uliyofanyika mjini Morogoro.
Mtakwimu Mohamed Kilonzo kutoka ofisi ya Taifa ya Takwimu akiwaelekeza wahariri na waandishi wa habari waandamizi jinsi ya kujaza dodoso refu litakalojazwa wakati wa sensa ya watu na makazi inatarajia kufanyika kote nchini kuanzia tarehe 26 Mwezi wa nane mwaka huu. Wanahabari hao walihudhuria mkutano wa siku moja wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 iliyofanyika jana mjini Morogoro.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...