Mkuu wa Wilaya ya Mvomero,Mh. Anthony Mtaka (katikati) ambaye alikuwa ni mgeni rasmi kwenye Sherehe za utoaji wa Zawadi kwa Washindi wa Tuzo za Excel With Grand Malt 2012 kwa vyuo vya Mzumbe na Sokoine vya Mkoani Morogoro,akizungumza machache kabla ya kuanza kwa zoezi la utoaji wa zawadi hizo kwa washindi mbali mbali walioshiriki kikamilifu kwenye shindano hilo.Sherehe hizo zimefanyika jioni hii kwenye viwanja vya michezo vya Chuo Kikuu cha Mzumbe Mkoani Morogoro.Kulia ni Meneja kinywaji cha Grand Malt ambao ndio wadhamini wakuu wa Tuzo hizo,Consolata Adam na Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha Mzunge,Prof. Faustin Kamuzola.
 Meneja kinywaji cha Grand Malt ambao ndio wadhamini wakuu wa Tuzo Excel With Grand Malt 2012,Consolata Adam akitoa shukrani zake kwa Vyuo vyote vilivyoweza kushiriki katika Mashindano hayo muda mfupi kabla ya kuanza kwa zoezi la utoaji wa zawadi hizo leo.
 Kaimu Mkuu wa Chuo cha Mzunge,Prof. Faustin Kamuzola (kushoto) akizungumza wakati wa sherehe hizo.
 Washindi mbali mbali wa tuzo za Excel With Grand Malt kutoka Vyuo vya Mzumbe na Sokoine wakiwa katika Picha ya Pamoja na Viongozi wa Vyuo hivyo,Wafanyakazi wa kampuni ya Bia ya Tanzania (TBL) na Mgeni Rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, wakionyesha fedha zao walizoshinda mara baada kukabidhiwa jioni ya leo kwenye viwanja vya Chuo Kikuu cha Mzumbe.
 Prof Jay ndie alieweza kusindikiza Shereha za utoaji wa Tuzo hizo kwa mapini yake makali makali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...