Bondia Francis Cheka (katikati) akitamba mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) kuwa atamchakaza mpinzani wake Japhet Kaseba.

WAKATI homa ya mapambano ya ndondi yanayosubiriwa kwa hamu kati ya Francis Cheka na Japhet Kaseba pamoja na wakali wa filamu nchini, Wema Sepetu na Jacqueline Wolper, ikizidi kupanda, baadhi ya mabondia hao wametoa tambo kuwa watawachakaza wapinzani wao siku hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari asubuhi ya leo kwenye hoteli ya kisasa ya The Atriums jijini Dar, Jacqueline Wolper alitamba kumpiga vibaya mpinzani wake siku ya Jumamosi kwenye Tamasha la Matumaini pale Uwanja wa Taifa.

“Sipendi maneno, napenda vitendo, nimekuwa nikisikia Wema na rafiki yake wanaongea sana kuhusu mimi kwenye TV.

“Nataka nikate mdomo wake siku hiyo kwa kumpiga" alisema Wolper. Nae Bondia Francis Cheka alitamba kuwa kama kawaida yake atamchachafya mpinzani wake katika tamasha hilo.
(PICHA/HABARI : ERICK EVARIST/GPL)

Wolper (kulia) akijitapa kuwa atamtwanga mpinzani wake mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani).
Nahodha wa Bongo Fleva, H Baba (kulia) akiahidi ushindi kwa timu yake dhidi ya Bongo Movie.
Hafla hiyo ilihudhuriwa pia na (kutoka kushoto) kocha wa bondia Francis Cheka (Abdalah Saleh Komando), Francis Cheka, meneja wa mfuko wa elimu (Charles Kapima), mmoja wa waratibu wa tamasha hilo (Luqman Maloto), promota wa pambano hilo, Kaike Silaju, bondia Japhet Kaseba na mwisho ni meneja wa Kaseba (Idd Bakari).
Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 06, 2012

    Mbese tuwakilishe mwana...mpe makonde huyo cheka.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 06, 2012

    samahani wadau mimi sijaelewa,
    Wolper na Wema nao watapigana boxing au vipi,tafadhali nielewesheni

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 06, 2012

    Pambano la wema na wolper, global publishers ulaji wataliandika mwaka mzima na kwa kila staili, hatimaye hawa wadada wanaweza pambana tena kavukavu nje ya ulingo. subirini muone

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 07, 2012

    Hata mimi sijaelewa kwani hawa nao ni mabondia na wameanza kini? mimi najua ni waigizaji tafadhali tujuzeni imekaaje hii?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...