Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) Anna Mkapa(kulia) na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Mwanaidi Sinare-Majaar(kulia kwa Mama Mkapa) wakiangalia aina ya vipodozi vilivyotengenezwa kutokana na mimea ya asili jana jijini Dar es salaam wakati Balozi huyo alipotembelea banda la EOTF . Kushoto ni Meneja wa Masoko na Mauzo kutoka Equator Natural Comestics ya Jijini Dar es salaam Anna Mnaya.
EOTF imeendelea kuwa mstari wa mbele katika kuendeleza wajasiriamali kinamama kwa mafunzo ya mbinu za kisasa ya kutengeneza, kupakia na kuuza bidhaa wanazotengeneza wenyewe ambapo mamia ya kinamama wamenufaika sana na taasisi hiyo. Kwa takriban miaka 10 sasa EOTF imekuwa ikiandaa mabanda maalumu ya kinamama wajasiriamali katika maonesho hayo ya SABASABA kila mwaka.
















































Post a Comment