Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) Anna Mkapa(kulia) na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mwanaidi Majaar(kulia kwa Mama Mkapa) wakiangalia aina ya vipodozi vilivyotengenezwa kutokana na mimea ya asili jana jijini Dar es salaam wakati Balozi huyo alipotembelea banda la EOTF . Kushoto ni Meneja wa Masoko na Mauzo kutoka Equator Natural Comestics ya Jijini Dar es salaam Anna Mnaya.
Afisa Mauzo wa Benki ya Posta Christina Mselewa(kulia) akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea Banda la Wizara ya Fedha jinsi ya kujaza fomu za kujiunga na Benki hiyoakati wa Maonyesho ya 36 ya Kimataifa ya Dar es salaam yanayoendelea katika viwaanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Mjumbe wa Bodi ya Mfuko wa Akiba ya Wafanyakazi Serikalini Joyce Shaidi ( wa pili kutoka kushoto)akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea mfuko huo jana jijini Dar es salaam wakati alipotembelea banda la Wizara ya Fedha katika maonyesho ya 36 ya Dar es salaam yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu J.K Nyerere.
Afisa Mawasiliano wa Wizara ya Fedha Fredrick Mbonde akitoa ufafanuzi jana jijini Dar es salaam kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na Wizara hiyo katika kumwendeleza mwananchi . Afisa huyo alitoa maelezo hayo wakati wa Maonyesho ya 36 ya Kimataifa ya Dar es salaam yanayoendelea katika viwaanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.Picha na MAELEZO - DAR ES SALAAM.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...