Rais Jakaya Kikwete akitoa hotuba yake kushukuru msaada magari 11 ulioyatolewa na Mkurugenzi wa Frankfurt Zoological Society (FZS) kanda ya Afrika, Robert Muir kwa ajili ya kupambana na vitendo vya ujangili katika hifadhi za Serengeti, Selous na Maswa.
Rais Jakaya Kikwete wa pili kushoto akipata maelezo kuhusu msaada wa magari 11 kutoka kwa Mkurugenzi wa Frankfurt Zoological Society (FZS) kanda ya Afrika, Robert Muir (katikati)na kulia ni Balozi wa Ujerumani nchini Hans Koeppel katika hafla iliyofanyika leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Msaada huo umetolewa na FZS kwa ajili ya kupambana na vitendo vya ujangili katika hifadhi za Serengeti Selous na Maswa.Mkurugenzi wa Frankfurt Zoological Society (FZS) kanda ya Afrika, Robert Muir(katikati) akitoa hotuba yake kuhusu msaada magari 11 waliyoyatoa kwa ajili ya kupambana na vitendo vya ujangili katika hifadhi za Serengeti ,Selous na Maswa,kushoto wa pili ni Rais Jakaya Kikwete na wa kwanza ni Balozi wa Ujerumani nchini Hans Koeppel na kulia wa pili Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu.Rais Jakaya Kikwete wa pili kushoto akionesha moja ya ufunguo wa msaada wa magari 11 mara baada ya kukabidhiwa na Mkurugenzi wa Frankfurt Zoological Society (FZS) kanda ya Afrika, Robert Muir ( kulia wanne) katika hafla iliyofanyika leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Msaada huo umetolewa na FZS kwa ajili ya kupambana na vitendo vya ujangili katika hifadhi za Serengeti ,Selous na Maswa.Balozi wa Ujerumani nchini Hans Koeppel akizungumza jamabo wakati wa hafla hiyo iliyofanyika leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na Magreth Kinabo -MAELEZO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Kumbe ujangili huu una madhara na kwenye Elimu(tafiti za kielimu),akili yangu yote yote ilikuwa kwenye ecosystem na utalii.Na zina thamani gani hizo "DIFENDA" 11??Offcourse, tunaelewa zina msamaha wa kodi.Pongezi kwa FZS.Lakini hawa Wajerumani walitunyonya bwana ingawa walituachia miundo mbinu

    David V

    ReplyDelete
  2. Tupambane na majangili ilituokoe hifadhi zetu na utalii wa mbuga za wanyama kwa ujumla wake.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...