Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe wakiongea na watoto Samir Juma (fulana nyekundu) na Salum Chumu wakiwa katika pantoni la MV Magogoni wakivuka kuelekea Kigamboni jijini Dar es salaam leo April 17, 2014. Watoto hao ambao wanasoma darasa la awali katika shule ya msingi ya Bunge, walipata bahati ya kuketi na viongozi hao waliokuwa wakielekea kuhani msiba wa kada wa CCM Marehemu Edward Masanja Ng'hwani maeneo ya Kibada.
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na watoto Samir Juma (fulana nyekundu) na Salum Chumu wakiwa katika pantoni la MV Magogoni wakivuka kuelekea Kigamboni jijini Dar es salaam leo April 17, 2014. Watoto hao ambao wanasoma darasala awali katika shule ya msingi ya Bunge, walipata bahati ya kuketi na na baadaye kutelemka na Rais aliyekuwa akielekea kuhani msiba wa kada wa CCM na mwenyekiti wa Washirika Kitaifa mstaafu Marehemu Edward Masanja Ng'hwani maeneo ya Kibada.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo alipokwenda kuhani na kutoa heshima za mwisho kwenye msiba wa kada wa CCM na mwenyekiti wa Washirika kitaifa mstaafu Marehemu Edward Masanja Ng'hwani maeneo ya Kibada jijini Dar es salaam leo April 17, 2014.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa kada wa CCM na mwenyekiti wa Washirika kitaifa mstaafu Marehemu Edward Masanja Ng'hwani maeneo ya Kibada jijini Dar es salaam leo April 17, 2014.PICHA NA IKULU. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Big up, Mr JK, how you mage this I really don`t know, kuendesha Nchi na kwenda kuhani kwenye misiba, mi-stew naona nimekukumbusha a few daya ago matumizi ya "kuhani" licha ya kwamba nipo mamtoni > 20 yrs.Thanks bro.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...