Kijana
aliyetambulika kwa jina la Musa Mbeko(24) anayedaiwa kuwa ni mwandishi
wa habari mkoani Tabora akiwa mikononi mwa Jeshi la Polisi mkoani humo
baada ya kujifanya kuwa ni afisa kutoka idara ya usalama wa taifa
(TISS). Kijana huyo inadaiwa aliwahi kufanya kazi kituo cha radio cha
Voice of Tabora (VOT) kinachomilikiwa na mbunge wa Jimbo la Tabora
mjini, Mhe. Ismail Aden Rage. Hata hivyo Uongozi wa VOT umekana kijana huyo kuwa ni
mwandishi wao na kwamba ulikwisha mfukuza kazi kutokana na makosa mbalimbali
yakiwemo ya tuhuma za utapeli
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Suzan Kaganda akiwaonesha waandishi wa
habari kitambulisho kilichokuwa kikitumiwa na Mussa Mbeko akijifanya ni
Afisa Usalama wa Taifa.
.
Kijana Musa Mbeko akiwa mbele ya kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Suzana Kaganda.
Kijana Musa Mbeko akiwa chini ya Ulinzi
So Sad. Si wamsaidie tu ajiunge na idara kama yeye ndo anaifia hiyo kazi!!! Maana nadhani ataifanya kwa umahiri sana kwani ndo ndoto yake pengine. Pole kijana usiwe unadanganya. Kote duniani ukiwa mwongo utajikuta katika hali mbaya. Jifunze kutoka kosa hili.
ReplyDeleteVijana siku hizi ndo imekuwa deal, mnatusumbua sana huko kwenye mabaa kidogo tu unanijua mimi nitakupoteza ooh, huyu sasa naye ameshindwa hata kujitambua mana hicho kitambulisho kimechanganywa lugha si mchezo, hapo kwen=li ni Tabora mwanawane mh
ReplyDelete