Na Rose Masaka MAELEZO-Dar es Salaam
TAASISI ya Hawzat Imam Swadiq wameandaa maandamano ya kulaani mashambulizi yanayofanywa na Vikosi vya Israel dhidi ya wananchi wa Palestina wasio na hatia.
Kwa mujibu wa Msemaji wa Taasisi hiyo Profesa Abdul Shariff, maandamano hayo yanalenga kuueleza ulimwengu kuwa wananchi wa Tanzania wanalaani mauaji yanayoendelea huko Gaza Palestina.
Amesema kuwa maandamano hayo ambayo yatafanyika siku ya Ijumaa Julai 25 mwaka huu yanatarajia kuanzia Kituo cha Daladala cha Boma na kuishia Kigogo uwanja wa Bibo.
Profesa Shariff ameongeza kuwa wameamua kupaza sauti zao kulaani baada ya kuona Jumuiya mbalimbali za Kimataifa ikiwa imenyamaza huku mamia ya watu wakizi kupoteza maisha yao.
Amesema kuwa inasikitisha kuona hata vyombo vya habari hasa vya Magharibi havitoi nafasi kubwa kwa mauaji hayo ukilinganisha na mauaji yaliyotokea kwa kulipuliwa kwa ndege Malyasia.
Naye Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Sheikh Hamed Jalala amesema kuwa wamealika viongozi na Mabalozi wa Nchi mbalimbali ili nao waweze kushiriki katika kupaza sauti zao pamoja na watanzania kulaani vitendo vinavyofanywa na Israel vya kuua watu wasio na hatia.
Sheikh Jalala amesema kuwa kunyamazia tatizo hilo ni kufanya kosa kwani hakuna hata dini moja inaruhusu mauaji ya binadamu mwingine.
Amesema kuwa maandamano hayo yatahusisha watu wa dini zote na yamepata Kibali cha Mamlaka husika.
Michuzi usibanie hii.
ReplyDeleteCha kushangaza hao wapalestina kwa siku wanafyatua makombora zaidi ya 1000 Israel. Licha ya kuwa Israel ina technologia ya kuyazuia lakini Wapalestina wakipewa mkongoto wanatafuta huruma ya dunia. Israel inawatafuta Hamas ambao wanajificha uraiani na wanatumia raia wa kawaida kama kinga. Vilevile wanavyowafyatulia Waislaeli makombora siyo yadondokee kwenye makambi ya jeshi bali uraiani yakauwe raia wa Isarael wasio na hatia. Unazi huu wa kushabikia ujinga hautupeleki popote. Mbona Wapalestina wa Ramallah wanakula kuku kwani toka enzi za Arafat walikubalian na Waislaeli. Bwana Profesa profesi amani kuliko kushabikia.
Shut up wee anonymous wa hapo juu. Mambo ya ngoswe muachie mwenyewe
ReplyDeleteshutup na wewe anonymous, kama ya Ngoswe wamuachie Ngoswe, hata hawa wanaoandamana wangekaa ndani !
ReplyDelete