Mganga
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt. John Gurisha akipimwa kabla ya kuchangia
damu katika zoezi lilioendeshwa na Shrika la Red Cross katika kuchangia
damu Mkoani Rukwa. Kumekuwepo na uhaba mkubwa wa damu katika Hospitali
Kuu ya Mkoa wa Rukwa na vituo vingine uhaba ambao unafikia nusu kwa nusu
ukilinganisha kiasi kinachopatikana na mahitaji yaliyopo. Uhaba huo
umesababishwa na muamko hafifu wa wananchi kuchangia damu kutokana na
hofu inayosababishwa na dhana potofu kuwa uchangiaji damu una madhara
kwa mchangiaji. Madaktari hao wa Hosptali Kuu ya Mkoa pamoja na
watumishi wengine wa Serikali waliamua kujitolea ili kuonyesha mfano kwa
wananchi waweze kuondokana na hofu hiyo waweze kujitokeza kuchangia
damu kuokoa maisha ya watanzania wanaohitaji huduma hiyo muhimu.
Baadhi ya madaktari wa Hospitali Kuu ya Mkoa wa Rukwa wkichangia damu.
Muuguzi Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Esther Kasegezya akichangia damu katika zoezi hilo.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Rukwa Dkt. Samwel Marwa akipatiwa vipimo muda mfupi kabla ya kuchangia damu.
Dkt. Marwa akichangia damu.
Mchangiaji baada kutoa damu hupata viburudisho ikiwemo vinywaji baridi na biskuti maalum.
Sehemu ya damu iliyokuwa imechangiwa katika zoezi hilo.
Picha na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...