Na Rose Masaka - MAELEZO

WANANCHI mkoani Lindi wanatarajiwa kuelimishwa njia bora na za kisasa za uvuvi, ufugaji na ukulima ili waweze kuboresha kipato chao na Taifa kwa ujumla. Kauli hiyo imetolewa leo mjini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wakulima Tanzania(TASO) Engelbert Moyo wakati akiongea na waandishi wa habari.

Amesema kuwa wakati wa maonesho ya nanenane ambayo Kitaifa yanafanyika mkoani Lindi watajitahidi kuhakikisha wananchi wanajifunza teknolojia mpya za kilimo, ufugaji na uvuvi ili waweze kuzalisha mazao yanayokidhi viwango vya Kitaifa na Kimataifa.

Moyo ameongeza kuwa watawaelimu wavuvi juu ya madhara ya uvuvi haramu na unavyohatarisha mazingira na viumbe wa majini.

Aidha Mwenyekiti huyo amesema kuwa maonesho yatafunguliwa na Rais wa Serikali za Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein na kufungwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.

Amesema kuwa Mawaziri mbalimbali watasaidia kutoa elimu kwa wakazi wa Mkoa huo kuhusu shughuli mbalimbali wanazozifanya katika kuwaletea maendeleo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...