27 Agosti, 2014, Dar es Salaam, Tanzania–BG Tanzania ilia​ndaa ​hafla kwa ajili ya kuwaaga wanafunzi kumi watanzania wali​o​faulu kupata udhamini wa elimu ya juu ngazi ya stashahada ya uzamili ( Masters of science degree ) ya sayansi kwenye vyuo vikuu nchini Uingereza.

Katika hafla hii, wanafunzi watapata fursa ya kukutana na Meneja Mkuu wa BG Tanzania ( Derek Hudson) pamoja na wafanyakazi na wadau Mbalimbali.

Udhamini huu wa elimu ya juu ni kati ya mpango mkakati wa maendelo ya jamii wa kampuni ya BG Tanzania. Mpango huu unatoa fursa sawa kwa watanzania na taratibu za kutahini na kupata wanafunzi zinafanyika kwa njia ya uwazi na umakini kuhakikisha fursa iliyopo inatolewa kwa wale wenye sifa na kukidhi vigezo. Wanafunzi wote wataenda kusoma kozi zinazohusiana na masuala ya gesi na mafuta kwenye vyuo vya Aberdeen na Robert Gordon.

Mpango huu wa udhamini wa elimu ya juu ulianza mwaka 2012 ambapo wanafunzi 4 hadi sasa wameishafaidi kwenye mpango huu. wanafunzi 2 waliishamaliza masono nakurudi nchini na 2 wanarudi mwishoni mwa mwaka huu.

Kwa kuzingataia umuhimu wa mpango huu, kwa mwaka 2014, BG Tanzania imeongeza udhamini kutoka wanafunzi 4 hadi 10 na idadi hii itaendelea kwa miaka 3.( wanafunzi 30 kufikia 2017) British Council wanatekeleza mradi huu kwa niaba ya BG Tanzania. Ufadhili unaotolewa ni kwa ajili ya ada, usafiri wa kwenda na kurudi, gharama za kuishi, gharama za mafunzo kwa vitendo. Kampuni ya BG itatoa fursa ya wanafunzi kutembelea makao makuu ya BG yaliyoko mji wa Reading- Uingereza ​. ​

Akiongea katika hafra hii, Meneja mkuu wa BG Tanzania, Bwana .Derek Hudson alisema, lengo la udhamini huu ni kuongeza idadi ya Watanzania wenye taaluma ya masuala ya gesi na mafuta nchini. Ni matarajio yetu kuwa, baada ya wanafunzi kumaliza watarudi kusaidia taifa kwa njia moja ama nyingine. BG Tanzania itaendelea kufanya kazi kwa karibu sana na serikali pamoja na wadau wengine kuhakikisha fursa hii inaongezeka iwezekanavyo
Meneja Mkuu wa BG Tanzania,Derek Hudson (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla hiyo ya kuwaaga wanafunzi kumi watanzania wali​o​faulu kupata udhamini wa elimu ya juu ngazi ya stashahada ya uzamili ( Masters of science degree ) ya sayansi kwenye vyuo vikuu nchini Uingereza. Kulia ni Mkurugenzi wa British Council nchini,Bw.Richard Sunderland.
Meneja Mkuu wa BG Tanzania Derek Hudson akiwa na wanafunzi waliodhaminiwa kupata elimu ya juu ya stashahada ya uzamili.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Vipi!
    Mbona hakuna majina ya wanafunzi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...