Na Faki Mjaka Maelezo Zanzibar

Wizara ya Afya Zanzibar imekabidhi kifaa cha THERMAL SCANNER kwa ajili ya kuchunguza Wagonjwa wa EBOLA watakao ingia nchini kutoka mataifa mengine.

Kifaa hicho kilichowekwa katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume kitatumika kwa ajili ya kuwachunguza zaidi Wageni ambao watatoka katika nchi zilizoathiriwa na Ugonjwa wa Ebola.

Akikabidhi kifaa hicho Mkuu wa kitengo cha kufuatilia mwenendo wa Maradhi Zanzibar Dkt Salma Masauni amesema THEMO SKAN kitasaidia katika kuwabaini watu ambao wameathirika au kuwa na dalili za Ungojwa wa Ebola na kuchukuliwa hatua zaidi.

Dkt Salma amesema iwapo mgonjwa atabainika hatua zaidi zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kupelekwa katika kituo cha Afya cha Chumbuni ambacho kimetayarishwa kwa ajili hiyo.

Aidha Dkt Salma amefahamisha kuwa Kituo cha Afya cha Chumbuni kimetengwa kama eneo litakalotumika kwa ajili ya Matibabu kwa mgonjwa atakayebainika kuambukizwa Ugonjwa wa Ebola nchini.

Amesema Wizara ya Afya katika kukabiliana na Ugonjwa huo wa kuambukiza imekuwa ikifanya Jitihada mbalimbali za kutoa elimu na njia mbali mbali za kinga kabla ya Zanzibar kuathirika na Ebola.

Amesema licha ya Vifaa hivyo vilivyotolewa Vifaa vingine vitakuja wiki inayokuja ili viendelee kutumika katika maeneo ya Bandarini na Viwanja vya ndege Unguja na Pemba

Dkt. Salma amesema Ugonjwa huo haujaingia nchini bali Serikali inajiandaa na juhudi zake za kukabiliana na Ugonjwa huo ili usiweze kuingia na kuathiri Zanzibar.
Mkuu wa kitengo cha kufuatilia mwenendo wa Maradhi Zanzibar Dkt Salma Masauni akionesha Kifaa “THERMAL SCANNER” kwa Wafanyakazi wa Kituo cha Afya cha Uwanja wa ndege wa Zanzibar. Kifaa hicho kitatumika kusaidia kuwabaini Wagonjwa wa EBOLA watakao ingia nchini kutoka mataifa mengine.
Mkuu wa kitengo cha kufuatilia mwenendo wa Maradhi Zanzibar Dkt Salma Masauni na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhamiaji Zanzibar wakionesha baadhi ya Vifaa Vitalavyotumika kuwachunguza Wagonjwa wa EBOLA watakao ingia nchini kutoka mataifa mengine.
Mkuu wa kitengo cha kufuatilia mwenendo wa Maradhi Zanzibar Dkt Salma Masauni akionesha matumizi ya Kifaa cha “THERMAL SCANNER” kwa Wafanyakazi wa Kituo cha Afya cha Uwanja wa ndege wa Zanzibar. Kifaa hicho kitatumika kusaidia kuwabaini Wagonjwa wa EBOLA watakao ingia nchini kutoka mataifa mengine.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hii inatia huruma. Sasa ilibidi kwa wanaopima kuvaa nguo zinazozuia kuambukizwa kwa ebola. Sasa ukimpima mtu unagundua kuwa anaebola na hujavaa nguo za kujikinga utafanyaje?


    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...