Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb.), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (wa tatu kutoka kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mawaziri saba wa Mambo ya Nje wa Nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara wakiwa na mwenyeji wa Mkutano huo Waziri wa Mambo ya Nje wa Singapore Mhe. Kasiviswanathan Shanmugam (wa tano kutoka kushoto).
Mawaziri wa Mambo ya Nje wakiwa kwenye ziara kwenye mojawapo ya vyuo maalum nchini humo Institute of Technical Education ambapo Tanzania inashirikiana nacho kwenye kutoa mafunzo kwa walimu wa VETA.
Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (kushoto) akikata utepe kufungua rasmi ofisi za Ubalozi wa Heshima za Tanzania nchini Singapore akishirikiana na Mhe. S.S. Teo, Balozi wa Heshima. Kulia ni Mhe. John Kijazi, Balozi wa Tanzania nchini India ambaye pia anaiwakilisha Tanzania nchini Singapore.
Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (wa pili kushoto), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwa kwenye picha ya pamoja na Mhe. John Kijazi (wa kwanza kushoto), Balozi wa Tanzania nchini India ambaye pia anaiwakilisha Tanzania nchini Singapore, Mhe.S.S. Teo, Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Singapore na Balozi Mbelwa Kairuki, Murugenzi wa Idara ya Asia na Australasia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (wa pili kushoto), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwa kwenye picha ya pamoja na Mhe. Kasiviswanathan Shanmugam, Waziri wa Mambo ya Nje wa Singapore (wa tatu kushoto), Balozi Mbelwa Kairuki na Mhe. John Kijazi, Balozi wa Tanzania nchini India na Singapore.
Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwa kwenye mazungumzo na mwenyeji wa Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara Mhe. Kasiviswanathan Shanmugam, Waziri wa Mambo ya Nje wa Singapore.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...