Wiki hii imekuwa njema kwa mustakabali wa jimbo la Darfur ambalo kwa muda mrefu limeshuhudia mgogoro wa wenyewe kwa wenyewe. Hizi ni taarifa za kujumuishwa kwa waasi wa zamani wa kikundi cha JEM-SUDAN kwenye jeshi la kitaifa nchini Sudan kufuatia hatua ya kikundi hicho kutia saini makubaliano ya Doha kuhusu amani Darfur.

Kwa mujibu wa Ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika huko Darfur, UNAMID umesema hilo ni kundi la kwanza kutoka takribani askari 2700 ambao hatimaye watajiunga na jeshi la kawaida.

Kufuatia hatua hiyo Joseph Msami wa idhaa hii amezungumza na Mkuu wa vikosi vya UNAMID Luteni Jenerali Paul Mella na kwanza amenza kumuuliza wamepokeaje hatua hiyo.

(SAUTI MAHOJIANO)
Kusikiliza bofya hapo chini

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...