Katibu wa Bunge Maalum la Katiba Mhe. Yahya Khamis Hamad akiongea na waandishi wa Habari kuhusu uwasilishwaji wa Sura zilizosalia za Rasimu ya Katiba Mpya utakaofanywa na Kamati zote 12 za Bunge. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Itifaki wa Bunge hilo, Bw. Jossey Mwasyuka. Mkutano huo ulifanyika Septemba 1, 2014 kwenye Ukumbi wa Spika mjini Dodoma.
Baadhi ya Waaandishi wa Habari wakifuatilia kwa makini taarifa ikiyotolewa na Katibu wa Bunge Maalum la Katiba wakati wa mkutano huo ulifanyika 01 Septemba, 2014 kwenye Ukumbi wa Spika mjini Dodoma.


KAMATI 12 za Bunge Maalum la Katiba kesho zitaanza kuwasilisha Sura zilizosalia za Rasimu ya Katiba Mpya ambazo ni Sura ya Pili, Tatu, Nne na ya Tano kwa mujibu wa ratiba iliyopangwa tangu tarehe 5 Agosti, Mwaka huu.
Hayo yamesemwa leo na Katibu wa Bunge Maalum la Katiba Yahya Khamis Hamad wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habri kwenye Ukumbi wa Spika mjini Dodoma.
“Kila Kamati imeshandaa taarifa kwa ajili ya kuiwasilisha katika Bunge hapo kesho”, alisema Katibu huyo.
Aidha, Katibu huyo ameongeza kuwa baada ya sura hizo kumalizika, Sura zitakazofuata ni Sura ya Saba, Nane na 14 na nyingine ni sura mpya.
Ameongeza zaidi kuwa, utaratibu huo utaendelea mpaka sura zote zitakapomalizika siku ya tarehe 8 Septemba, 2014 saa mbili usiku.
Katibu ameongeza kuwa Bunge hilo litaanza kujadili Sura hizo za Rasimu ya Katiba Mpya kuanzia siku ya tarehe 9 Septemba, 2014.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...