Mkuu wa Magereza Mkoani Morogoro, Naibu Kamishna wa Magereza, James Selestine(wa kwanza kushoto) akiteta jambo na Watendaji Waandamizi wa Shirika la Magereza na GEPF kabla ya kutembelea katika eneo la Kihonda, Morogoro ambapo mradi wa Majengo ya vitega uchumi kwa ubia kati ya Shirika la Magereza na GEPF utakapojengwa(wa kwanza kulia) ni Mkurugenzi wa Uwekezaji, Bw. Festo Fute(wa pili kulia) ni Mtendaji Mkuu wa Shirika la Magereza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, John Masunga.
 Watendaji Wakuu wa Shirika la Magereza, GEPF na Wataalam Washauri wakiendelea na Kikao kazi katika eneo la Kihonda, Mkoani Morogoro ambapo mradi wa Majengo ya vitega uchumi utakapojengwa kama inavyoonekana katika picha.
Mkuu wa Gereza Kihonda, Mkoani Morogoro, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Ben Mwansasu akiwaonesha eneo la Uwekezaji Watendaji Wandamizi wa GEPF na Wataalam washauri walipotembelea eneo hilo leo Agosti 1, 2014 Mkoani Morogoro. Jeshi la Magereza kupitia Shirika lake la Magereza limeingia Makubaliano ya ubia na Mfuko wa Jamii wa GEPF katika miradi ya ujenzi wa Majengo ya vitega uchumi katika eneo la Karanga, Kilimanjaro na Kihonda Mkoani Morogoro.
 Msanifu wa Majengo toka Kampuni CONS AFRIKA ya Jijini Dar es Salaam, Bw. Henry Mwoleka(wa kwanza kushoto) akisisitiza jambo muhimu wakati Watendaji wa Shirika la Magereza, GEPF na Wataalam washauri walipotembelea eneo la Uwekezaji la Kihonda, Mkoani Morogoro ambapo mradi wa Majengo ya vitega uchumi utafanyika. Timu hiyo ya Wataalam imeendelea na Kikao chake leo Agosti 1, 2014 Mkoani Morogoro(wa pili kulia) ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Morogoro, Naibu Kamishna wa Magereza, James Selestine(wa pili kushoto) ni Mtendaji Mkuu wa Shirika la Magereza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, John Masunga wakisikiliza maelezo ya Msanifu Majengo wa Kampuni ya CONS AFRIKA ya Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Magereza Mkoani Morogoro, Naibu Kamishna wa Magereza, James Selestine akiwa katika picha ya pamoja na Watendaji Waandamizi wa Shirika la Magereza, GEPF na Wataalam washauri mara tu baada ya kikao kazi cha kupitia na kuangalia maeneo ya Uwekezaji katika miradi ya vitega uchumi utakaofanyika. Kikao hicho kimeendelea leo Agosti 1, 2014 Mkoani Morogoro(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
========  ====== =========
Na; Lucas Mboje

Kikao kazi cha Watendaji Wakuu wa Shirika la Magereza, Mfuko wa Jamii wa GEPF na Wataalam Washauri kimeendelea leo Agosti 1, 2014 Mkoani Morogoro. Lengo la Kikao hicho ni kupitia na kuangalia maeneo ambayo Uwekezaji katika mradi wa Majengo ya vitega uchumi utafanyika.

Kikao hicho ni sehemu ya maandalizi ya mwanzo ya kuanza shughuli rasmi za ujenzi wa Majengo ya vitega uchumi kwa ubia kati ya Jeshi la Magereza kupitia Shirika lake la Uzalishaji mali(Prisons Corporation Sole) na Mfuko wa Jamii wa GEPF.

Mpango huu wa ujenzi wa Majengo ya vitega uchumi unatarajiwa kuanza mapema mwishoni mwa Mwaka 2014 mara baada ya kukamilika kwa michoro na mahitaji mengine muhimu ambapo unatarajiwa kutekelezwa katika maeneo ya Jeshi la Magereza ya Kihonda Mkoani Morogoro na Karanga - Moshi Kilimanjaro.

Tayari, Jeshi la Magereza nchini kupitia Shirika lake la Uzalishaji Mali limetiliana Mkataba wa Uwekezaji wa Mfuko wa Jamii wa GEPF ambapo Majengo ya vitega uchumi yatajengwa katika maeneo ya Kihonda Mkoani Morogoro na Karanga - Moshi Mkoani Kilimanjaro. Utiwaji sahini ya Mkataba huo ulifanyika Mei 29, 2014 katika Ukumbi wa Mikutano ulioko Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Dar es Salaam.

Kupitia ubia huo Shirika la Magereza litapata pato ambalo litaimarisha zaidi upanuaji wa shughuli za miradi ya Shirika hilo sambamba na kuipunguzia gharama Serikali.

Jeshi la Magereza kupitia Shirika lake tayari limefikia makubaliano na Wawekezaji mbalimbali wa ndani na nje ya nchi ambao wamevutiwa na shughuli za kiuwekezaji kwa lengo la kuingia ubia hivyo kukuza mitaji na kubadilishana ujuzi katika miradi mbalimbali ikiwemo ya Madini na Kilimo katika maeneo ya Jeshi la Magereza.

Wakati huo huo, Jeshi la Magereza Tanzania Bara lipo katika maandalizi ya mwisho ya kuzindua TOVUTI yake ambapo kupitia Tovuti hiyo itarahisisha Mawasiliano pia Wananchi na Wadau mbalimbali watapata taarifa muhimu kuhusiana na Jeshi hilo. Tovuti hiyo itapatikana kupitia akaunti ya Anuani ya www.magereza.go.tz.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...