Mwenyekiti wa Kikundi cha Tumaini Saccos, akiowanesha namna sanduku maalumu la kutunzia taarifa za kikundi chao linavyolindwa, wakati maofisa wa Kampuni ya Bia Tanzania walipokwenda hivi karibuni kukagua miradi mbalimbali ya wananchi wilayani Arumeru inayowezeshwa na Taasisi ya ACE AFRIKA kwa ufadhili wa TBL.
 Mwanachama wa Tumaini Saccos ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa kikundi hicho akionesha baadhi ya shughuli anazozifanya mbazo amewezeshwa na ACE AFRICA  chini ya ufadhili wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL). Maofisa wa TBL walikwenda hivi karibuni kukagua miradi ya kikundi hicho.
 Mkulima wa bustani ya ndizi na mboga za majani, Isaya Supuk wa kijiji cha Olmotonyi, wilayani Arumeru, Arusha akiwaonesha maofisa wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) na ACE AFRICA namna shamba lake lilivyostawi wakati maofisa hao wa TBL walipokwenda hivi karibuni kukagua shughuli hizo zilizofadhiliwa na na kampuni hiyo.
Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),  Editha Mushi akizungumza na Mkurugenzi wa ACE AFRICA (TANZANIA), Joanna Waddington ofisini kwake Arusha, hivi karibuni kuhusu ufadhili wao unaowezeshwa na taasisi hiyo kwa wananchi wa Arumeru katika shuguli mbalimbali za maendeleo.. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hahahaha kwani kuweka kufuli nyingi mtaji?

    Watu wanalivunja sanduku kwa Shoka la Umsolopagas ama linavunjwa kwa kulipuliwa na baruti na hapo michuzi yote inakombwa!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...