Afisa lishe wa Wilaya ya Njombe akitoa mada
kwenye semina ya maafisa watendajji wa kata na viongozi wa vijiji wakati wa
semina kuhusu kuongeza virutubishi kwenye vyakula iliyofanyika wilayani humo
katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Njombe leo.Kampeni za matumizi ya
vyakula vyenye virutubishi zinaendelea katika wilaya mbalimbali nchini.
Wanakijiji cha Ngalanga wilayani Njombe
wakisikiliza mtaalamu wa lishe wa wilaya Bi Bertha Nyigu wakati wa semina juu
ya matumizi ya vyakula vilivyoongezewa virutubishi iliyofanyika katika viwanja
vya halmashauri ya wilaya ya Njombe.Kampeni za matumizi ya vyakula vyenye
virutubishi zinaendelea katika wilaya mbalimbali chini ya usimamizi wa Wizara
ya Afya na Ustawi wa jamii na wadau wengine wa masuala ya afya.
Mtaalamu wa
masuala ya lishe wa wilaya ya Njombe,Bi Bertha Nyigu, akijibu maswali ya
wanavijiji mbalimbali waliofika kupata elimu ya masuala ya lishe na uongozeji
virutubishi kwenye chakula.Kampeni za lishe bora na virutubishi zinaendelea
kufanyika katika wilaya mbalimbali hapa nchini chini ya usimamizi wa Wizara ya
Afya na Ustawi wa Jamii.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...