Mkurugenzi  wa Covenant Bank,  Mama Sabetha Mwambenja, akimpokea  Waziri  wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dr, Titus Kamani, wakati akiwasili katika hafla ya kukabidhi Ng’ombe 83 wa Maziwa kwa wafugaji wadogo wa Kikundi cha Somangira walioko Kigamboni Jijini Dar es Salaam, Ng’ombe hao wamenunuliwa kwa Mkopo kutoka Covenant Bank.
 Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dr. Titus Kamani, akizungumza na wananchi wa kijiji cha Somangira, Kigamboni Jijini Dar es Salaam katika hafla ya kukabidhi  Ng’ombe 83 wa maziwa kwa kikundi wafugaji wadogo wa kijiji hicho Ng’ombe hao wamenunuliwa kwa Mkopo kutoka Covenant Bank. Pamoja nae katika Picha ni Mkurugenzi wa Covenant  Bank. Sabetha Mwambenja. 
 Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dr. Titus Kamani, akikamua Maziwa kutoka kwa moja ya Ng’ombe 83 wa Maziwa, punde baada ya Kuwakabidhi kwa wafugaji wa kikundi cha Somangira – Kigamboni jijini Dar es Salaam, wanaoshuhudia ni Mratibu wa Kikundi hicho Bibi. Getrude Mpelembe(kushoto)  Mkurugenzi wa Covenant Bank. Bibi Sabetha Mwambenja (Katikati) na Mwenyekiti wa Wajasiriamali wasio katika Sekta Rasmi, Dauda Salmin.
: Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dr. Titus Kamani, akikabidhi moja ya Ng’ombe 83 wa Maziwa, kwa Bibi. Robi Chacha ambaye ni miongoni mwa wanakikundi 83 waliokabidhiwa Ng’ombe hao ambao wamenunuliwa kwa Mkopo na Covenant Bank. Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi wa Covenant Bank. Sabetha Mwambenja, (Mwenye miwani katikati) na Mwenyekiti wa Wajasiriamali wasio katika Sekta Rasmi Dauda Salmin

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...