Mwalimu Masungwe Revania akiwa anaendelea na matibabu  katika chumba cha upasuaji katika hospital ya Mkoa wa Kigoma maweni baada ya kulipukiwa na jiko la gesi na kumuunguza vibaya.

Picha na habari na Editha Karlo
wa Globy ya Jamii, Kigoma
Mwalimu wa shule ya sekondari ya mazungwe Revania Ndebigeze(39)Wilaya ya Uvinza Mkoani hapa amelazwa katika hospital ya Mkoa wa Kigoma(Maweni)baada ya kuungua vibaya na moto wa gesi.

Akiongea na mwandishi wa habari hii kwa taabu katika chumba cha upasuaji mwalimu huyo alisema kuwa tukio hilo lilimkuta jumatatu majira ya saa tano asubuhi wakati akijiandaa na mapishi nyumbani kwake.Alisema kuwa alikuwa ametoka kazini na kupita kwenye maduka ya gesi kigoma mjini  na kununua gesi na kupewa maelekezo yote na wataalum ya jinsi ya kuitumia gesi hiyo.
Alipofika nyumbani aliungaunisha gesi hiyo na jiko ili aweze kutumia lakini alishindwa na kumuita mwalimu mwenake amsadie lakini naye alishindwa kufanikiwa kuliwasha jiko hilo.
''Niliamua kujaribu tena kuliwasha mwenyewe kulinga na maelezo niliyopewa na taalamu wakati na nunua nikafanikiwa kuliwasha lakini haikupita dakika tano nikasikia harufu ya tofauti nikaamua kwenda kulizima ndo likalipuka na kuniunguza ''alisema mwalimu huyo kwa masikitiko.
Alisema baada ya gesi kulipuuka na kumuunguza majirani walimpeleka katika zahanati ya jirani ya mazungwe ambapo alipatiwa rufaa ya kwenda hospita ya rufaa ya maweni anapopatiwa matibabu mpaka sasa.Mwalimu huyo ameungua vibaya sehemu za usoni, miguu yote na mikono yote,mabega,mikono,
Daktari wa zamu Dkt Fadhili Kabaya alisema hali ya mgonjwa inaendelea vizuri.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. POLE SANA MUNGU ATAKUSAIDIA.
    KWA UTAALAMU WANGU WAKATI UNAUNGANISHA GASI KTK JIKO LAKO HAUWEKA VIZURI KTK CONTAKT ,NA HIYO NDO SABABU YA GASI KURIPUKA ILE HARUFU NI GASI YAKO ILIKUWA INAVUJA
    WATUMIAJ WA MAJIKO YA GESI INABID MUOMBE MAFUNZO ZAID KWANI INATIA URUMA KWA YANAYOTOKEA , NA UKIZINGATIA HOSPITALI ZETU HUYO DADA ATABAKI NA KILEMA MAISHA

    ReplyDelete
  2. Ni kwamba, siku zote ukisikia harufu ya gas cha kwanza, usiguse kabisa kabisa kile kibiriti cha kuwashia maana kile cheche moja tu inalipua kila kitu, toa ule mpira kwenye kitako cha mtungi, au zimia pale pale kwenye kitako cha mtungi wa gas, halafu fungua milango yote, madirisha nk toka nje na toa watoto, na jamaa. Hakikisha hakuna hata mtu mmoja anapita anavuta sigara au lala. ile hewa ikisha isha ndani sasa ingia na rudisha kile kibiriti kwenye sehemu yake. na tafuta mtaalamu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwani linawashwaje jaman

      Delete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...