Balozi wa kujitolea wa kampeni ya mapambano dhidi ya mauaji ya albino, Henry Mdimu (wa pili kulia) akizungumza na vyombo vya jhabari. Kampeni hiyo inajulikana kwa jina la Imetosha. Balozi wa kujitolea wa kampeni ya mapambano dhidi ya mauaji ya albino, Henry Mdimu (wa pili kulia) akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es salaam. Kampeni hiyo inajulikana kwa jina la Imetosha.Mchoraji maarufu na mmoja wa wanakamati wa kampeni za imetosha Masoud Kipanya (kulia) akizungumza na DW. Mchoraji maarufu na mmoja wa wanakamati wa kampeni za imetosha Masoud Kipanya (kulia) akizungumza na DW.Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN), Joachim Mushi (kulia)  akihojiwa na DW mara baada ya mkutano wao. TBN imeunga mkono kampeni hizo zinazoongozwa na balozi wa kujitolea wa mapambano hayo, Henry Mdimu. Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN), Joachim Mushi (kushoto) akihojiwa na DW mara baada ya mkutano wao. TBN imeunga mkono kampeni hizo zinazoongozwa na balozi wa kujitolea wa mapambano hayo, Henry Mdimu.Baadhi ya wajumbe wa kampeni za imetosha wakipata picha za ukumbusho mara baada ya kuzungumza na wanahabari. Baadhi ya wajumbe wa kampeni za imetosha wakipata picha za ukumbusho mara baada ya kuzungumza na wanahabari.Mkutano na wanahabari ukiendelea. Mkutano na wanahabari ukiendelea wakati Henry Mdimu akifafanua jambo kushoto kwake ni Masoud Kipanya

  Na TBN
  MMOJA wa watu wenye ulemavu wa ngozi  na mwanahabari shupavu kutoka kampuni ya Mwananchi Communication, Henry Mdimu amejitolea kuwa balozi wa hiyari kupinga mauaji ya kikatili ya watu wenye albino yanaoendelea nchini. 
 Bw. Mdimu ambaye ameungwa mkono na baadhi ya marafiki na watu wanaokerwa na vitendo hivyo, ikiwemo Chama cha Bloggers nchini, Tanzania Bloggers Network (TBN) amesema ameamua kufanya hivyo baada ya kushuhudia ndugu zake wakiteseka kwa muda mrefu dhidi ya mauaji hayo. 
 Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Balozi Mdimu amesema lengo lake kuu ni kuhakikisha anazunguka pamoja na marafiki watakao muunga mkono na kutoa elimu kwa kuanzia Kanda ya Ziwa ili tatizo hilo lisiendelee kuenea nchi nzima. 
 Akifafanua zaidi alisema mauaji ya watu wenye albino yanaichafua Tanzania hivyo atahakikisha anaisaidia Serikali kupambana na watu wenye imani hizo za kipuuzi ili kuondoa doa linaloichafua nchi yetu ambayo imekuwa na sifa ya amani dunia nzima. 
 "...Nimeamua kufanya hivi baada ya kushuhudia ndugu zangu wakiteseka kwa muda mrefu. Awali nilishindwa kuanzisha harakati hizi nikiamini kuna vyombo vinavyohusika na utetezi wa watu wenye ulemavu wa ngozi." "...Hivyo nimeamua niweke jitihada zangu binafsi niisaidie Serikali yangu katika kuondoa doa hili linaloichafua Nchi yetu yenye sifa ya Amani duninia nzima. Hivyo nawaomba Watanzania wenzangu mniunge mkono tukishirikiana na Serikali ili mauaji haya yakome," alisema Mdimu. 
 "Kutokana na ushawishi nilionao kama Mwandishi, Mtangazaji wa redio na Blogger naamini nitaleta mabadiliko makubwa katika kuhakikisha haki ya kusihi kwa ndugu zangu inaheshimiwa na kubaki historia. 
"Salamu zangu ziwafikie wanyanyasaji, wauaji na wenye kufanya dhihaka kwa watu wenye ulemavu wa ngozi kuwa IMETOSHA." 
 Akifafanua zaidi alisema kwa uchunguzi wake wa awali umebaini ukosefu wa elimu juu ya watu wenye ulemavu wa ngozi ndio chanzo cha tatizo hilo kukua na hatimaye kuuana kwa imani za kishirikina. 
"...Hivyo basi, silaha ya Elimu ni sehemu kubwa ya haraki hizi," alisisitiza Balozi huyo wa kujitolea. Aidha alisema kuendesha harakati hizo alizozipa jina la 'IMETOSHA' elimu itatolewa kwa njia ya sanaa, na washauri nasaha pamoja na kundi la wanamuziki ambao pia wataandaa nyimbo mbalimbali za kutoa mafunzo ya kutokomeza ukatili huu. Alisema wasanii ambao hadi sasa wamejitokeza kuunga mkono kampeni hizo ni paoma na Jhikoman, Kassim Mganga, Profesa J, Ray C, Fid Q, Roma Mkatoliki na Dami Msimamo. Hata hivyo alisema bado pia anaamini nguvu ya vyombo vya habari ikiungana na kampeni hizo wanaweza kufanikiwa zaidi hivyo kuomba ushirikiano katika kuhakikisha vinapaza sauti kutokomeza mauaji hayo ya kikatili. 
*Imeandaliwa na www.thehabari.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Mtangulize na maombi ya dini zote maana nguvu za giza mnazoenda kupambana nazo huko mnakoenda sio mchezo. Msiwasahau kuwashirikisha kabisa viongozi wa dini. Na hivi wanajua mnaenda watajiandaa, ni wazo tu kiroho safi.

    ReplyDelete
  2. Kweli pambana kabisa tupo nyuma yako tunakuombea. Tunapinga kabisa vitendo hivyo

    ReplyDelete
  3. Mawazo yako ni mazuri sana kaka Henry, Mwenyezi Mungu aliwezeshe hili lifanikiwe. Natambua kuwa ufinyu wa elimu wa watu wa ngazi ya chini ndo unaopelekea haya yote kutokea. Na waelimisheni kuwa hii ni Amri ya Mungu Usiue, na usiabudu Miungu ya uwongo? maana hizo Imani potofu ni sawa na kuabudu mashetani. Wamwogope Mungu wanaofanya hivyo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...