Na Editha Karlo, Globu ya Jamii - Kigoma

MKAZI wa Kijiji cha Buzebazeba katika Manispaa ya Kigoma Ujiji, Zuwena Abdu (29) jana amejifungua watoto mapacha wanne kwa mkupuo katika Hospital ya Mkoa  wa Kigoma (Maweni).

Zuwena alisema kuwa watoto aliojifungua wenye jinsia ya kiume ni  watatu na  mmoja ambaye ni wa mwisho ana jinsia ya kike ,wa kwanza akiwa na uzito wa kilo 1.8,pili 2.5 wa tatu 1.7 na wanne 1.7.

Alisema watoto hao alijifungua jana majira ya saa kumi na mbili jioni salama  kwa njia ya kawaida 

Zuwena alisema huo ni uzazi wake wa tano ambao awali alijifungua wanne kwa njia ya kawaida kwahiyo jumla anaidadi ya watoto nane.

''Kwanza nina mshukuru mungu kwa kuniwezesha kujifungua salama watoto wote na wakiwa hai kutokana na hali duni ya  kiuchumi ya familia yetu mimi na mume wangu tunaomba Watanzania wenye mapenzi mema watusaidie ili tuweze kuwalea hawa watoto,mume wangu hana kazi na mimi sina kazi''alisema mama huyo

Muuguzi wa zamu katika wodi  ya wazazi  Agness Nguvumali alisema kuwa alifikishwa mama huyo alifikishwa hospitalini hapo siku ya jumatatu saa kumi jioni akiwa na uchungu na ilipofika saa kumi na mbili akawa amejifungua mapacha wanne kwa njia ya kawaida salama.

Muuguzi huyo alisema kuwa watoto wote wana afya njema alisema wataendelea kubaki hospitalini hapo kwaajili ya uangalizi wa karibu wa madaktari.

Agness amewaomba Watanzania,mashirika mbalimbali kujitokeza kumsaidia mama huyo ili aweze kuhudumia watoto wake hao kwakuwa hali yake ya uchumi na mume wake siyo nzuri na utunzaji wa mapacha hao unahitaji uwezo wa nguvu ya ziada.
 YEYOTE MWENYE MSAADA KWA WATOTO HAO ANAWEZA KUWASILIANA KWA KUTUMIA NAMBA 0752202783
Mama wa watoto mapacha wanne, Bi. Zuwena Abdu akiwa wodini baada ya kujifungua.
Muuguzi wa zamu katika Wodi ya wazazi ya Hospital ya Mkoa wa Kigoma (Maweni), Agness Nguvumali akiwaangalia mapacha wanne waliozaliwa hospitalini hapo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Jamani mbona aibu Tanzania kusikia
    mtu amejifungua watoto 4 asaidiwe nawanachi kweli USTAWI WA JAMII KAZI YAO NINIHILO NI JJUKUMU LA UTAWI WA JAMII KAZI YAO NDIO HIYO MSAIDIENI UTAWI WA JAMII

    ReplyDelete
  2. HUYU MAMA HANA MUME?

    ReplyDelete
  3. mtu mpaka akatoka kwenye kadamnasi anaomba msaada inamaana kuwa hata kama ana mume au ustawi wa jamii wapo yeye bado anahitaji msaada, kama huna au hutaki kutoa ni bora ungekaa kimya au angalau mpongeza kwa kupata watoto wanne wenye afya.

    ReplyDelete
  4. Umeambiwa mume wake hana uwezo,soma habari vizuri.

    ReplyDelete
  5. Si imeandikwa hapo kuwa mume hana kazi, tunaishi katika nyakati ambazo nchini kwetu mume anaweza kuwa hana kazi. Ndiyo maana ni vizuri mama na baba tuchakalike. Ni vizuri wilaya atokako impatie angalau shamba kama hana mahali pa kulima. Kulima pia ni kazi, kwa sababu kumsaidia kujisimamia kimapato ili aweze kutunza watoto nane ni vizuri zaidi kuliko tu umpatia msaada wa mara moja peke yake. Wasanii Kigoma njoo mtikite kumsaidia mama huyu.

    ReplyDelete
  6. Duuh! Kwanza alikua ana watoto wanne! akataka kuongeza mmoja nae amekuja na wenzie��! watoto ni Baraka lakini tuangalie hili ' vipato vyetu viendane na idadi ya watoto tunao wazaa' . Tutumie uzazi wa mpango. Tunalalamika maisha magumu bado tunataka watto wengi. Tunawatunzaje hawa watoto? Tubadilike

    ReplyDelete
  7. Hongera Dada yangu wala usijali kila kijacho ALLAH anatanguliza rizki yake.

    ReplyDelete
  8. Hongera Dada yangu wala usijali kila kijacho ALLAH
    anatanguliza rizki yake.

    ReplyDelete
  9. BWANA MICHUZI WEKA UTARATIBU AU SIMAMIA HIYO SHOO kuna watu hawajatoa sadaka muda mrefu nina imani tunaweza kusaidia...
    kwa ufupi watoto hao wote hawawezi kulala kwa wakati mmoja, hivi wakiamua kulia wote anafanyaje,kunyonyesha je? ni changamoto kubwa si mchezo...tumsaidie

    ReplyDelete
  10. Yeye hana kazi, mume hana kazi na tayarii ana watoto 4 ..hivi ni kitu gani kilichomfanya atake ongeza watoto wengine? Matatizo mengine ni ya kujitakiaa, kwani uzazi wa mpango hajui! !?lol..wanawake kama hawa wanahitaji Elimu ya kutoshaa otherwise in two years atabeba mimba tenaa! !!! Halafu ataomba msaada tena, huyu mama inabidi asaidiwe halafu apewe elimu ya uzazi wa mpango..yeye na mumewe piaa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...