Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano unaozungumzia jinsi ya kupata Maendeleo endelevu kwa kukuza ajira na kazi zenye utu (Achieving sustainable development through employment creation and decent work) tarehe 30 Aprili, 2015 katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (UN) jijini New York, Marekani.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake wakiondoka baada ya yeye kuhutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano unaozungumzia jinsi ya kupata Maendeleo endelevu kwa kukuza ajira na kazi zenye utu (Achieving sustainable development through employment creation and decent work) tarehe 30 Aprili, 2015 katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (UN) jijini New York, Marekani.

=====  ======  ======
Kuna Umuhimu mkubwa wa kuweka suala la Ajira  katika  ajenda   ya maendeleo,  mipango na progamu ya Mataifa yote duniani.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete amesema hayo tarehe 30 Aprili, 2015 katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (UN) jijini New York wakati wa ufunguzi wa Mkutano  unaozungumzia jinsi ya kupata Maendeleo endelevu kwa kukuza ajira na kazi zenye utu  (Achieving sustainable development through employment creation and decent work).

Rais Kikwete amesema tatizo la ajira lina pande mbili, kwanza linaweza kutumika vizuri pale  wawekezaji wanapokuja  barani Afrika, wanaweza kupata nguvu kazi iliyopo tayari,  ikiwa inakidhi matakwa ya kazi na pili ni changamoto kubwa pale ambapo ajira hazipatikani kwa kundi kubwa la vijana ambao wanaongezeka kila mwaka.

"Hivyo ni muhimu ukuzaji wa ajira kuwa kipengele muhimu katika ajenda ya maendeleo, mipango na programu mbalimbali katika Mataifa yote" Rais amesema na kuelezea kuwa pamoja na ukweli uliopo kuwa nchi mbalimbali barani Afrika ikiwemo Tanzania, zimeonyesha hali nzuri ya uchumi kwa miongo miwili mpaka mitatu iliyopita, na kuonyesha kuwa bara la Afrika ni moja ya mabara yanayokua kwa kasi kiuchumi duniani, bado bara linakabiliwa na tatizo kubwa la ajira. 

"Natarajia  tutabadilishana mawazo ya jinsi gani Afrika inaweza kutatua tatizo hili na pia kupata mawazo ya nini kifanyike kuweza kuvutia wawekezaji zaidi". Rais amesema. 


"Pia nitapenda kupata mawazo na ikiwezekana kuunga mkono katika kusaidia vijana wetu katika suala la kujiajiri" ameongeza na kusema suala hili linahitaji programu maalum na miradi. 

Rais Kikwete amezungumzia suala la ajira barani Afrika kuwa la kutia mashaka na hivyo kuhitaji hatua za haraka. Takwimu zinaonesha kuwa Afrika ilitengeneza ajira 37 million  pekee kwa kipindi cha muongo uliopita, kati ya hizi asilimia 28 zilikuwa ajira zenye utu, na wakati huo huo inakadiriwa kuwa, soko la ajira barani Afrika linapokea watu milioni 122 katika ajira mpya kila mwaka. 

"Hii inatisha sana kwa vile karibu watu 200 barani Afrika ni wake wenye miaka 15 na 24 na kwamba idadi hii itaongezeka mara mbili ifikapo mwaka 2045" 
Rais amefafanua na kuonyesha wasiwasi wake kwamba bara la Afrika litakumbwa na idadi kubwa ya ukosefu wa ajira, na kibaya zaidi idadi kubwa kuwa ya vijana.

Imetolewa na; 
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
New York - USA
31 Aprili, 2015

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Kazi za kuajiriwa katika nchi za Afrika zitakuwa tu kama sera ya binafsi itapanuka uwekezaji utaongezeka na juhudi za kuwezesha wote kuchangia katika uchumi zitafanikiwa. Ajira ni uwezo wa kuzalisha na kulipa mishahara, kama uzalishaji wa huduma ama bidhaa haupo basi uwezo wa kulipa mishahara unapungua. Vijana kufikiria kujiajiri pia ni jambo muhimu ikiwa ni pamoja na kuwekeza kwenye kilimo kwetu sisi tuliojaliwa ardhi yenye rutuba.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...