Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Pangani, Saleh Pamba bungeni mjini Dodoma Aprili 1,2015.. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Naibu Waziri Wizara Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Mhe.Pindi Chana akijibu swali la msingi la Mhe.Kidawa Salehe (Mb) Viti Maalum CCM lililohoji juu ya Serikali imefanya utafiti gani juu ya sababu za ukatili kwa watoto,bungeni Mjini Dodoma 1 Aprili,2015.
Mbunge wa Kisarawe (CCM) Mhe.Seleman Jafo akiwasilisha hoja binafsi kuomba tarehe ya kura ya maoni isogezwe mbele na kupendekeza Serikali ipeleke Muswada Bungeni wa hati ya dharura kupitisha Katiba ya mpito,Bungeni Mjini Dodoma 1 Aprili,2015 .
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akitoka nje ya ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma mara baada ya kuhairisha bunge kutokana na fujo zilizozuka ndani ya bunge kutoka na kuwepo kwa mwingiliano wa hoja binafsi kati ya Mhe.Seleman Jafo (Mb) CCM Kisarawe na Mhe.John Mnyika (Mb)Ubungo CHADEMA Bungeni Mjini Dodoma 1 Aprili,2015.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Bunge linakwenda vizuri lakini kinachowakasirisha hata wanachini, ni kile kisemwacho na mpinzani ni kibaya, tunakosea sana maana hata wapinzani wamekwenda shule ndiyo maana hata kwenye uchangiaji wanachangia sana tena sana kuliko hata chama tawala, kazi kusema ndiyo tu wasijue ni kibaya au kizuri. hapa tunaharibu nchi yetu, bora waangalie yaliyo mazuri wachukueni siyo yote ni mabaya

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...