Marehemu Dkt. Alec 
Chemponda enzi za uhai wake

Mwenyekiti Mtendaji wa Michuzi Media Group anaungana na familia, ndugu, jamaa, jirani na marafiki wa  Chemponda katika kuomboleza kifo cha Dkt Alec Che Mponda kilichotokea juzi Machi 30, 2015 katika hospitali ya Massana jijini Dar es salaam kutokana na saratani (cancer) ya mifupa iliyokuwa ikimsumbua kwa muda mrefu. Alikuwa na umri wa miaka 80.

Tunatoa mkono wa pole kwa binti mkubwa wa marehemu na blogger na mwanahabari mwenzetu, Bi Chemi Che-Mponda pamoja na wadogo wake wote na wajukuu wa marehemu ambaye atakumbukwa kuwa mmoja wa wanasiasa wakongwe nchini aliyepata kuanzisha na kuongoza chama cha Tanzania People'e Party (TPP).

Mbali na siasa pamoja na kuwa mmoja wa watangazaji wa kwanza wa Idha ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika (VOA) Marehemu Dkt Che-Mponda pia aliandika thesis ya shahada ya uzamivu (PhD) juu ya mzozo wa mpaka wa Tanzania na Malawi ambayo imesimama kama kimoja ya kielelezo muhimu katika swala hilo nyeti.

Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa marehemu Mbezi (mbele ya Massana Hospital) jijini Dar es salaam.

Mola aiweke roho ya marehemu 
mahala pema peponi
Amen


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Pole Chemi na Jessica. mungu amlaze mzee mahali pema peponi. Amina.

    ReplyDelete
  2. Poleni wafiwa Mungu awatie nguvu wakati huu mnapoomboleza kuondokewa na mpendwa wenu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...