Uelewa finyu juu ya masuala ya utoaji wa mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu umeendelea kuwa chanzo cha baadhi ya wahitaji wa mikopo kulalamika bila kuanza kutafuta chanzo cha wao kutopata mikopo hiyo.

Hayo yamebainika hii leo katika ziara ya mafunzo ya wanachuo 147 kutoka Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) unaoendeshea shughuli zake Bagamoyo mkoani Pwani waliofika Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kwa ziara ya mafunzo.

Miongoni mwa maswali yaliyoulizwa na wanachuo hao ni pamoja na uwezekano wa wafanyakazi kupatiwa mikopo, vigezo vya utoaji mikopo na jinsi ya kubaini waombaji wa mikopo wenye sifa za kupata mikopo hiyo. Maswali mengine yalilenga kujua jinsi Bodi inavyowatambua wanufaika wa mikopo ambao mikopo yao imeiva tayari kurejeshwa.

Awali, Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano Bw. Cosmas Mwaisobwa aliwasilisha mada iliyojumuisha historia fupi ya Bodi, Sera ya Uchangiaji, Muundo wa Uongozi, Utaratibu wa Utoaji Mikopo na Utaratibu wa Urejeshwaji wa mikopo ya elimu ya juu.

Akitoa shukrani kwa niaba ya wanachuo hao, Mkufunzi aliyeandamana nao Bibi Rhoda Samwepa, ameelezea kufurahishwa kwake na jinsi Bw. Mwaisobwa ambaye pia ni Msemaji wa Bodi, alivyotolea ufafanuzi kwa ufasaha masuala yanayoonekana kuwa na utata kuhusu mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu na kwamba anaona umuhimu wa wanufaika kurejesha mikopo hiyo ili wahitaji wengine waweze kunufaika.

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu imekuwa ikipokea makundi mbalimbali ya wadau wa elimu wanaofika kwa lengo la kujifunza masuala ya utoaji mikopo, vigezo na masharti ya utoaji mikopo na utaratibu wa kurejesha mikopo hiyo na hivyo kuendelea kuongeza uelewa wa mikopo ya wanafunzi kwa idadi kubwa zaidi ya wadau.
Sehemu ya wanachuo wa ADEM wakimsikiliza Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano Bw. Cosmas Mwaisobwa (haonekani kwenye picha hii).
Baadhi ya wanafunzi wa ADEM wakifuatilia kwa makini mada iliyokuwa ikiwasilishwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano Bw. Cosmas Mwaisobwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...