Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt  John Pombe Magufuli na Mgombea Mwenza Ndugu Samia Suluhu Hassan wakionesha fomu zao za kuomba kugombea urais mara baada ya kuchukua kwenye ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi jijini Dar es salaam leo, ambapo walisindikizwa na viongozi mbalimbali pamoja na wanachama wa CCM na wananchi kwa ujumla wakiwa wamepanda kwenye gari maalum.
 Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dkt John Pombe Magufuli na Mgombea Mwenza Mhe Samia Suluhu Hassan wakionesha mkoba wenye fomu za Kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama hicho mbele ya wananchi  na wanachama wao nje ya ofisi ndogo ya CCM Mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam baada ya kutoka Tume ya Uchaguzi kuchukua Fomu za kugombea Urais  leo agosti 4, 2015.
  Mwenyekiti wa CCM Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwashukuru wananchi na Wanachama wa chama hicho walioshiriki shughuli nzima ya kumsindikiza Dkt John Pombe Magufuli ya kuchukua fomu ya kuwania kiti cha Urais kupitia chama hicho katika ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi jijini Dar leo.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana akiwashukuru Wananchi na wafuasi wa chama cha CCM walioshiriki shughuli nzima ya kumsindikiza Dkt John Pombe Magufuli ya kuchukua fomu ya kuwania kiti cha Urais kupitia chama hicho katika ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi jijini Dar leo.
 Mhe Samia Suluhu Hassan akiwashukuru Wananchi na Wanachama wa CCM waliojitokeza kwa wingi nje ya ofisi ndogo ya CCM Mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam baada ya kutoka Tume ya Uchaguzi kuchukua Fomu za kugombea Urais leo agosti 4, 2015.
Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dkt John Pombe Magufuli na Mgombea Mwenza Mhe Samia Suluhu Hassan nwakilakiwa na Mwenyekiti wa CCM Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wengine akipokewa katika ofisi ndogo ya CCM Mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam baada ya kutoka Tume ya Uchaguzi kuchukua Fomu za kugombea Urais leo agosti 4, 2015.
Picha ya pamoja
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akiwa sambamba na Katibu wa Itikadi na Uenezi  Taifa Nape Nnauye,Mwenyekiti wa CCM Mkoa Dar es Salaam,Ndugu Ramadhan Madabiba pamoja na pichani shoto Ndugu Januari Makamba aliyeshinda kura za maoni CCM jimbo la Bumbuli kwa pamoja wakimsindikiza Dkt Jonh Pombe Magufuli kuchukua fomu za kuwania Urais mapema leo jijini Dar. 
Wafuasi wa chama cha Mapinduzi wakiwa wamekusanyika nje ya Ofisi Ndogo ya Makao ya CCM mtaa Lumbumba wakishangwekwa wakati Mgombea Mteule wa Urais kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli aliyekuwa akienda kuchukua Fomu ya kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),jijini Dar leo. 
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Tunawatakia ushindi mkubwa na mafanikio mtakapoanza kampeni ya nchi nzima.

    ReplyDelete


  2. JPM FOR PRESIDENT !


    CCM HAPA MMEWAPIGA BAO WAPINZANI! TUMEUONA UTENDAJI WAKO KIONGOZI.
    HUO UMATI MKUBWA HAKUNA MICHUZI LINE, IT IS GENUINE.

    "CHAMA TAWALA" DODOMA BIG UP. MNGEVURUNDA KWENYE KUMPATA HUYO MNGETUANGUSHA WATZ WENYE LOGICAL THINKING.

    YOU GAVE US THE MOST SUITABLE, 'CLEAN', ETHICAL, WITH A CONSTRUCTIVE BRUTAL DRIVE.
    I ONCE HEARD THIS, AND I WAS DISSAPOINTED ON THAT REASONONG. ETI MKALI!

    ReplyDelete
  3. CCM mtashinda bila wasi wasi .All the best

    ReplyDelete
  4. Brother Michuzi unaweza kutuwekea video ya hii event kama unayo? Tulio mbali tunafarijika kusikia walichosema hawa watarajiwa

    ReplyDelete
  5. CCM Mwaka huu mmefanya uchaguzi ambao watz hawakutarajia, mmeonesha kuwa fedha si kigezo cha kumpata mtu anayestahili kuongoza, bali ueledi, ujuzi, umahiri na uwezo wa kuchapa kazi ndio kipaumbele cha mgombea anayetakiwa.

    Big up sana, all the best Hon. Magufuli

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...