Na John Nditi, Morogoro

WABUNGE wanne wa zamani katika majimbo ya mkoa wa Morogoro wamefanikiwa kutetea nafasi zao kwenye uchaguzi wa kura za maoni zilizofanyika Augosti 1, mwaka huu nchini kote kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).

Walionusurika kwa kutetea nafasi zao ni Mbunge wa Jimbo la Ulanga Mashariki, Celina Kombani, Ulanga Magharibi , Dk Haji Mponda, Jimbo la Morogoro Mjini Abdulaziz Abood na Jimbo la Gairo , Ahmed Shabiby .

Wabunge walioanguka katika kura za maoni ni pamoja na Innocent Kalongeries Jimbo la Morogoro Kusini aliyepigwa mwereka na Prosper Mbena, ambaye ni Katibu wa Rais Jakaya Kikwete, kwa kupata kura 9, 548, na Kalongeries akipata kura 7,714 na kushika nafasi ya pili, nafasi ya tatu imenyakuliwa na Zuberi Mfaume kwa kura 2,607.

Jimbo hilo lilikuwa wagombea sita akiwemo anayemaliza muda wake Augosti 20, mwaka huu , Kalogeries, ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro.

Mbali na hao wengine walikuwa ni Kessy Mkambala aliyapata kura 1,269 Lwitiko Beregu kura 740 , Zuberi Mfaume alijipatia kura 607, na Sudi Mpili alijipatia kura 347 .

Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki, Mgombea Omary Mgumba ameshinda kura za maoni kwa kupata kura 4,193, akifuatiwa na Jamila Mohammed Taji kura 3,497 wakati mbunge aliyekuwa akitetea nafasi yake Dk Lucy Nkya akiambulia kura 2,357, Jimbo hilo lilikuwa na wagombea 14.

Majimbo mengine ambayo wabunge watetezi wameshindwa kutetea nafasi zao ni pamoja na Mvomero, Mikumi, Kilombero, wakati jimbo la Kilosa lilikuwa wazi baada ya mbunge wake anaye maliza muda wake Mustafa Mkulo kung’atuka kwa hiari yake na kuwapisha wengine.
Prosper Mbena siku aliporejesha fomu ya kuomba kuteuliwa nafasi ya Ubunge , ( kulia) ni Katibu wa CCM Wilaya ya Morogoro Vijijiji, Shaibu Mtawa.
Mgombea wa Ubunge aliyeshinda kura za maoni Jimbo la Morogoro Kusini, Prosper Mbena ( wa kwanza kushoto) akiwa pamoja na mshindani wake, Kalongeries ( shati la kawaida).
Mbena ( kushoto) akisililiza maelezo ya mmoja wa wagombea mwezake.
Mbena akisaini daftari la orodha ya wagombea waliochukua na kurudisha fomu .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...