Na Bashir Yakub.
Nilipoandika kuhusu namna ya kuunda kampuni kwa mujibu wa Sheria ya Makampuni sura ya 212 nilieleza pia kuwa unapokuwa umekamilisha usajili wa kampuni na umepata cheti cha usajili yapo mambo mengine ya kufanya kabla ya kuanza rasmi biashara.
Moja ya mambo hayo nilisema ukishapata cheti unatakiwa uende manispaa husika ukapate leseni ya biashara. Manispaa husika ni manispaa ambako ofisi ya kampuni yako itakuwa. Kitu kingine baada ya kupata cheti cha usajili ni kupata namba ya mlipa kodi (TIN). Ili kampuni ifanye biashara kisheria inatakiwa kuwa imepata namba hii.
Yawezekana wanahisa kila mmoja anayo namba yake ya mlipa kodi lakini namba hizo haziwezi kutumika kwakuwa ni za watu binafsi na si za kampuni. Kampuni inatakiwa ipate namba yake inayojitegemea. Halikadhalika kwa wanaoanzisha vikundi kwa mfano saccos, na asasi za kiraia( NGOs) nao wanatakiwa kuwa na namba ya mlipa kodi ya vikundi hivyo.
1.TIN NAMBA HUPATIKANA WAPI.
Mamlaka ya mapato Tanzania ( TRA) ndiyo mamlaka inayoshughulika na utoaji wa namba za mlipa kodi. Awali namba hizi zilikuwa zikitolewa makao makuu ya mamlaka ya mapato ambapo kwasasa katika kuboresha huduma wameweka ofisi za kikanda sehemu mbalimbali ambazo huhudumia wahitaji wa kanda husika kwa mfano kwa Dar es salaam eneo la ilala , buguruni, tabata, kariakoo ofisi zipo makutano ya Shaurimoyo badala ya mnazi mmoja au samora . Hata hivyo yapo maeneo mengine ambayo ofisi za kanda hazijawekwa kwa mfano mikoani ambapo wahitaji hulazimika kufuata huduma hii makao makuu ya mamlaka ya mapato.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...