Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon, akiwa na Mabalozi Macharia Kamau wa Kenya na David Donoghue wa Ireland wakati walipozungumza na waandishi wa habari kuelezea namna mchakato wa majadiliano yaliyokamilisha na hatimaye kupitishwa nan chi wanachama Tamko kuhusu Ajenda za Maendeleo Endelevu baada ya 2015. Tamko hilo lilipitishwa jumapili usiku. Mabalozi wao ndio waliosimamia mchakato mzima wa majadiliano hayo.
Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi, muda mfupi baada ya kuahirishwa mkutano kwa mapunziko mafupi hapo siku ya ijumaa usiku na kisha mkutano kuendelea tena hadi alfajiri ya Jumamosi, wakarejea tena mchana na kuendelea tena hadi usiku wa kuamkia jumapili na kuendelea jumpily mchana hadi usiku walilopitisha tamko hilo. Pamoja na naye Mkurungenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestin Mushy.
Afisa Mkuu Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Bw.Songelael Shilla ambaye amekuwa akisimamia mchakato wa majadiliano yaliyopelekea kupatika kwa ajenda mpya za maendeleo endelevu baada ya 2015, aliyeketi nyuma ni Dk. Lorah Madete kutoka Tume ya Mipango hii ilikuwa ni Ijumaa usiku.
Baaada ya majadiliano makali yaliyodumu kwa wiki mbili na wakati mwingine wajumbe kulazimika kukesha hadi asubuhi. Hatimaye nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, Jumapili usiku (Agosti mbili), wamepitisha kwa kauli moja, rasimu ya tamko kuhusu Agenda ya Malengo ya Maendeleo Endelevu 2015.
Katika kuhakikisha kwamba ilikuwa ni lazima tamko hilo likamilike na kupitishwa, wajumbe walilazimika kukesha ndani ya ukumbi wa mkutano kulikokuwa kukifanyika mkutano huo, wakipimzika kwa saa chache na kurejea tena na hatimaye kufanikisha kukamilishwa kwa raslimu hiyo siku ya jumapili majira ya usiku.
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiongozwa na Mwakilishi wa Kudumu Balozi Tuvako Manongi na Afisa Mkuu Bw. Shilla, kwa kushirikiana na wataalamu kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, wakiongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestin Mushy, Wataalamu kutoka Tume ya Rais Mipango, Tanzania Bara na Visiwani, Wizara ya Fedha na Asasi zisizo za Kiserikali, imeshiriki kikamilifu katika kipindi chote miaka miwili tangu kuanza kwa mchakato wa majadiliano hayo.
Tamko lilolopitishwa i Jumapili, itawasilishwa mbele ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa katika tarehe itakayopangwa kupitishwa rasmi.
Viongozi Wakuu wa Nchi na Serikali watapokea na kupitisha tamko hilo katika mkutano wao wa Kihistoria utakaofanyika mwezi ujao ( 25-27Septemba) hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.
Akionyesha kufurahishwa na kuridhika kwake baada ya wajumbe kupitisha tamko hilo , Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, licha ya kuwapongeza wajumbe kwa kazi kubwa , kujituma kwao na zaidi kupitisha rasimu hiyo kwa kauli moja, amesema anasubiri kwa hamu kuungana na Viongozi Wakuu wa Nchi na Serikali zaidi ya 150 na wawakilishi wengine katika mkutano wa kilele utakaopitisha za ajenda hizo za maendeleo endelevu kwa miaka 15 ijayo.
Akasema mchakato mzima wa majadiliano ya maandalizi ya tamko hilo ambao umedumu kwa miaka miwili umefanyika kwa mshikamano, weledi na ulikuwa shirikishi , ambapo hata makundi mbalimbali ya kijamii, yalishiriki kwa ukamilifu.
Ban Ki Moon, amesema, ajenda mpya za maendeleo endelevu ambazo zinachukua nafasi ya Malengo ya Maendeleo ya Millenia yanayofikia ukingoni mwaka huu, zinalenga katika kuwaondoa watu kutoka katika lindi la umaskini pasipo kumwacha yeyote.
“Napenda kuwapongeza nchi wanachama kwa uongozi wenu na kujituma kwenu, nawashukuru pia Mabalozi Macharia Kamau wa Kenya na David Donoghue wa Ireland kwa namna walivyoendesha na kuusimamia mchakato huo bila kuchoka na kwa kuonyesha ufundi mkubwa wa kidiplomasia ” amesema Ban Ki Moon.
Na kuongeza kwamba Ajenda hiyo iitwayo: "kubadili dunia yetu: ajenda ya mwaka 2030 kwa maendeleo endelevu" inajumuisha masuala yanayowahusu wote ikilenga pia kuhakikisha Amani, ufanisi na kubuni ubia unaojali watu na sayari duni.
Juhudi kubwa lakini utekelezaji vipi? Malengo ya milenia wametuuza. Ukweli maendeleo ni watu wenyewe tusitegemee misaaada!
ReplyDelete