Kampuni ya Airtel Tanzania imeipiga ‘tafu’ timu ya soka na netiboli ya waandishi wa habari za michezo nchini, Taswa SC kwa kuwapatia vifaa vya michezo. 
 Akizungumza katika makabidhiano hayo jana, Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando alisema kuwa kampuni yao inatambua mchango wa waandishi wa habari za michezo nchini katika kuendeleza michezo na kuamua kutoa vifaa vya michezo ambazo ni seti mbili za jezi na mipira. 
 Mmbando alisema kuwa mbali ya kuwa wadau wakubwa wa michezo, msaada huo ni moja ya muendelezo wao katika shughuli za kijamii. “Airtel Tanzania ni wadau wakubwa wa michezo na burudani, tumeshiriki katika shughuli mbali mbali ikiwa kuendesha michezo ya Airtel Rising Stars, tumeamua kuunga mkono juhudi za timu ya waandishi wa habari za michezo kuwakutanisha wana-habari na kushiriki katika mazoezi na mechi kwa ajili ya kuhamasisha vipaji na afya zao,” alisema Mmbando. 
 Mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto Omary aliishukuru Airtel Tanzania kwa msaada huo ambao umetokana na maombi yao kwa kampuni hiyo. Majuto alisema kuwa Taswa SC kwa kujua wadau wake, waliamua kuomba msaada wa vifaa hivyo na Airtel Tanzania kuwajali na kuchukua juhudi za haraka kutoa mchango wao. 
 “Tumeomba kwa kampuni nyingi, bado hatujapata majibu ya kukubaliwa au la, Airtel Tanzania imeonyesha mfano kwa kutusaidia kwa haraka sana, ni faraja kwetu, tunawaomba wengine waige mfano wao,” alisema Majuto. Alisema kuwa Taswa SC bado inakabiliwa na changamoto ya vifaa vingine kama viatu kwa timu zake za soka na netiboli na kuwaomba wadau wafikirie kuwasaidia. 
“ Tupo tayari kupokea vifaa vingine, timu inatakiwa kuwa na vifaa vya kutosha, jezi za aina mbalimbali, mipira ya mazoezi na mechi, hivyo kama kuna wadau wanataka kutusaidia, wasisite kufanya hivyo,” alisisitiza Majuto.

Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando akimkabithi vifaa vya michezo moja wa wachezaji wa timu ya Taswa Queens , Imani Makongoro mara baada ya Airtel kuchangia kwa vifaa hivyo kwa timu za mpira wa miguu na netiboli kwa timu za waandishi wa habari nchini. Akishuhudia katikati ni Mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto Omary


Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando akimkabithi vifaa vya michezo Mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto Omary, baada ya Airtel kuchangia kwa vifaa hivyo kwa timu za mpira wa miguu na netiboli kwa timu za waandishi wa habari nchini

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...