WAZIRI MKUU Majaliwa Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi maafisa watano na watumishi watatu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutokana na upotevu wa makontena 349 yenye thamani ya zaidi ya sh. bilioni 80/-.

Akizungumza na viongozi wa Mamlaka ya Bandari pamoja na viongozi wa TRA katika ziara ya kushtukiza leo mchana (Ijumaa, Novemba 27, 2015), Waziri Mkuu amewataka Kamishna Mkuu wa TRA, Bw. Rished Bade na Naibu Kamishna Mkuu wa TRA, Bw. Lusekelo Mwaseba wahahakikishe wanashirikiana na polisi kufuatilia upotevu huo na kwamba fedha hizo zinapatikana na zinarudi Serikalini.

Akitangaza uamuzi huo baada ya kufanya kikao na baadhi ya viongozi wa Serikali bandarini hapo, Waziri Mkuu aliwataja maafisa waliosimamishwa kazi kuwa ni Kamishna wa Forodha, Bw. Tiagi Masamaki na Mkuu wa Kituo cha Huduma kwa Wateja, Bw. Habibu Mponezya.

“Hawa wanasimamishwa kazi. IGP ninaagiza hawa watu wakamatwe na kuisaidia polisi. Hati zao za kusafiria zikamatwe na mali zao zikaguliwe kama zinaendana na utumishi wa umma,” alisema Waziri Mkuu.

Maafisa wengine waliosimamishwa kazi ni Mkuu wa kitengo cha TEHAMA, Bw. Haruni Mpande, Bw. Hamisi Ali Omari (hakutaja ni wa idara gani), na Mkuu wa Kitengo cha Bandari Kavu (ICD In-Charge), Bw. Eliachi Mrema. “Hawa wanasimamishwa kazi hadi uchunguzi utakapokamilika na pia wawe mikononi mwa polisi,” alisema.

Pia aliagiza watumishi watatu wa mamlaka hiyo wahamishwe kutoka Dar es Salaam na kupelekwa mikoani. Watumishi hao ni Bw. Anangisye Mtafya, Bw. Nsajigwa Mwandengele na Bw. Robert Nyoni.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amemwagiza Katibu Mkuu wa Hazina, Dk. Servacius Likwelile ambaye alikuwepo kwenye kikao hicho, kuhakikisha kuwa anapeleka wataalamu kutoka Wakala wa Serikali Mtandao (e-Govt) haraka iwezekanavyo ili wakakague mifumo ya taarifa na kubaini jinsi ambavyo wizi huo unafanyika.

“Ninataka uchunguzi uanze kufanyika mara moja, tafuteni njia ambazo zinatumika kama mianya ya wizi kutokea hapa bandarini hadi kwenye ICDs. Nataka hayo makontena yatafutwe hadi yajulikane yako wapi, na fedha hiyo ihakikishwe inarudi serikalini,” alisema.

Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Bw. Ernest Mangu, Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Florens Turuka, Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya DSM, Suleiman Kova, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari (TPA), Bw. Awadh Massawe na viongozi mbalimbali kutoka TRA na TPA.

Mapema akijibu maswali ya Waziri Mkuu, Kamishna Mkuu wa TRA, Bw. Bade alikiri kwamba kuna upotevu wa makontena ambao huwa unafanyika kati ya bandarini na ICDs na hasa ICD ya Ubungo. Akitoa ufafanuzi, alisema kwamba walifanya ukaguzi kwenye ICD moja na kukuta makontena 54 yamepotea kwa njia za wizi. “Hata hivyo, tulipoendelea na ukaguzi, namba iliongezeka na kufikia 327. Tunaendelea kufuatilia kwa kushirikiana na TAKUKURU. Mmiliki wa ICD ametakiwa kulipa faini sh. bilioni 12.6/- na ameshalipa sh. bilioni 2.4/-,” alifafanua.

Alipoulizwa na Waziri Mkuu kama ana majina ya watumishi wanaohusika na wizi huo, Bw. Bade akakiri kwamba anayo lakini siyo kwa wakati huo labda ayapate kutoka kwa wasaidizi wake. Ndipo Waziri Mkuu akamuonyesha orodha ya makontena 349 yenye taarifa zote hadi namba za magari yaliyobeba mizigo hiyo na Bw. Bade akakiri kwamba orodha hiyo ni ya kweli.

“Kwa utaratibu huo hatuwezi kufika, labda baadhi ya watu waondolewe kazini”. Ndipo akaanza kutaja majina ya maafisa hao waliosimamishwa kazi.
Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na uongozi wa TRA na TPA alipofanya ziara ya kustukiza Bandarini leo asubuhi.
 Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa akiongea na viongozi wa TRA na TPA
Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa akikabidhi orodha ya makontena yaliyopotea na ambayo TRA haina taarifa nazo
Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa akiagana na viongozi wa TRA na TPA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Sasa intelijensia imeanza kufanya kazi kwa kasi. Waziri Mkuu ana majina ya kontena..lakkni bandari haina majina hayo. Hii kasi ni mpya sana. Vyombo vya usalama sasa viko activated.

    ReplyDelete
  2. Jamani watanzania badilikeni. Business as usual imeisha.

    ReplyDelete
  3. Napiga vigeregere, tunangojea habari zaidi tuletee.
    Hawa jamaa walikuwa wadokoa mali za uma bila haya wala aibu
    The new boys are in town now, the thieves arrogance will be their downfall
    Just throw the book on them like a ton of bricks.

    ReplyDelete
  4. JAMANI HIII nchi sijui tulikuwa tunaenda wapi?? Mungu ni mwema siku zote hakika MUNGU uwalinde viongozi wetu kwa kazi nzuri sana. Jamani tulikuwa tunakosa huduma bora za kijamii kwa sababu ya watu wachache tu. HAPA KAZIII TU

    ReplyDelete
  5. FUKUZA WOOOTE HAO NI WEZI WANAJUANA MADILI WANAPIGA PAMOJA TRA NA TPA

    ReplyDelete
  6. Tanzania tuna pesa nyingi ila zinaliwa na wachache. Vyanzo vyake vya pesa vinatosha tusihitaji msaada wa pesa kutoka nje. Inakuwaje tuwe masikini wakati tuna bandari 6 (3 za bahari na 3 za maziwa)? Mungu amlinde Rais wetu Dk. John Pombe Magufuli na ajaalie wasaidizi wake wawe kama yeye. Big up pia kwa Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa na yeye ataiti hivyo hivyo.

    ReplyDelete
  7. Big up PM walizidi mnoooo

    ReplyDelete
  8. Big up PM. Nyie wawili na Mr President mnaweza

    ReplyDelete
  9. Style hii magorofa yataongezeka kweli, alafu et nchi maskini bado ten percent kwenye miradi ya serikali kwenye wilaya na mikoa

    ReplyDelete
  10. Kazi kama hivi ninamkumbuka hayati eduward moringe sokoine

    ReplyDelete
  11. Heheheee naona macho yamewatoka hawakutegemea kama msako ungewapitia mapemaa. Kontena ziko wapi? na ni Kontena za kina nani mm. Hapo unaweza kukuta na Kontena za raia wa kawaida zimetolewa wakagawa wanakojua wenyewe. Kimenukaa!! Leoo! Liende mbele fagio la chuma liende mbelee!

    ReplyDelete
  12. Serikali za mitaa mheshimiwa, huko kuna wezi wamejificha ndio maana miji yetu michafu manispaa haziwajibiki kipindupindu kinazidi kuenea.

    ReplyDelete
  13. Mheshimiwa Waziri Mkuu sehemu nyingine pale Wizara ya Ardhi wahudumu wa mapokez na watoa hudumai ni Miungu watu wanalipa jina baya serikali yetu.

    ReplyDelete
  14. kwa style hiyo muheshimiwa anafaa sana mungu akulinde na wabaya wote tutafika tuu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...