Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania, Mh. Dkt John Pombe Joseph Magufuli amemsimamisha kazi kuanzia leo tarehe 27 Nov. 2015, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ndugu Rished Bade kufuatia ziara ya kushtukiza ya Waziri Mkuu, Mh. Majaliwa Kasimu Majaliwa mapema leo asubuhi Bandarini jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akizungumza na waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari (hawapo pichani) kuhusu upotevu wa makontena zaidi ya 349 huku akiwa ameshika nyaraka yenye orodha ya makontena hayo.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akionesha nyaraka hiyo mbele ya waandishi wa habari waliofika kwenye mkutano huo.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue wakwanza kushoto akifafanua jambo mbele ya wanahabari.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. Muheshimiwa sana.. magu. Dual zipo mbele yako Allah ' akulinde....,
    radhi zote zile juu yake yako. Imaana ilikua too much' wezi wengi sana. Endelea na kazi na wanyonge tujione kama nasi watanzania., maana ilikua balaa. Dhulma tupu.

    ReplyDelete
  2. Duu makontena 300

    ReplyDelete
  3. BANDARI YA TANZANIA AU SOMALI .....AU MULIKUWA MKUU KUTOKA SOMALI NIFAHAMISHENI SIJAFAHAMU MIMI

    ReplyDelete
  4. Bade umechemsha kwani JPM alisema toka mwanzo hapa akzi tu, akaongea alipovamia wizara ya fedha kuhusu watu wenye uwezo na wanakwepa kulipa kodi lakini kwa takriban wiki mbili hivi inaonekana hamkulivalia nuga hili. Inafurahisha sana sasa bongo watu watanza kufanya kazi kwa bidii na kuthamini kazi. Hadi "laha".

    ReplyDelete
  5. apelekwe jela wamezidi kudhulumu, hakuna ujamaa hapa kazi tu .

    ReplyDelete
  6. Asante Baba! Kaza uzi, mkombozi wa nchi yetu. Tuko pamoja Na wewe ku kuombea Kwa Mwenyezi Mungu akupe afya njema uendelee Na kazi Yako Kama ulivyotuahidi Watanzania !

    ReplyDelete
  7. Hongera, sana Rais JPM endelea kubaini madudu watu walizoea magumashi. Allah akuongoze katka haki

    ReplyDelete
  8. Hongera sana Rais JPM endelea kubaini madudu watu walizoea magumashi. Allah akuongoze katka haki

    ReplyDelete
  9. Kabla hawa ndugu kuanza uchunguzi wa kuwasaka hao majizi, ndugu zangu waliokuwepo hapo awal walikuwa wapi? ama ndiyo walifumba macho na kuziba masikio
    This was sealing on an industrial scale
    Containa mia tatu zapotea,just like magic
    Itawasaidia kama wanapenda makande maana ndiyo enzi zetu yalikuwa main menu kule mwisho wa lami.

    ReplyDelete
  10. Hongera Magufuli. Hongera Wazari Mkuu. Tunawaombea msiogope. Taifa lote la watanzania wako pamoja nanyi. Ushauri. Fungeni CCTV sehemu zote za bandari kila kona na kwenye viwanja vya ndege na mipakani. Zote hizo ziunganishwe kwenye chumba kimoja cha Intelijensia ofisi ya Rais Ikulu na kwenye vyombo vyote vya usalama. Chumba hicho kitakuwa kina control kila movementi maeneo hayo.

    ReplyDelete
  11. Naamini mungu anasikia,namuomba awalinde viongozi hawa kwa kiasi kile zilivyo dhamira zao katika kuirekebisha
    Katika makosa tunayotakiwa kujifunza watanzania ni kuchagua viongozi kwa ushabiki bila kuzingatia mahitaji yetu,kwa hilo huwa tunatenda kosa kubwa mno kuliko hata wale wanaokwapua mapesa yale.
    Hebu tuzinduke nasi ili viongozi kama hawa tusiwakatishe tamaa wakasema aah tunahangaikia majitu hayajitambui tutateseka bure hebu tuanze kivyetu,na ndipo mambo huharibika.
    Kila mtu ana mchango katika ustawi wetu-tutimize wajibu ipasavyo4

    ReplyDelete
  12. Hongera sana magufuli watu wote lazima walipe kodi. Hakuna kujuana matajiri wanatakikana kulipa zaidi but tz maskini wanalipa kodi matajiri halipi. No wanazidi kutakarika mtu ana mradi mdogo tra wanamzungukia paka basi hii dhulma.

    ReplyDelete
  13. mheshimiwa hawa watu ni mchezo wao kila siku, ofisi ilikuwa kama private business yao, walikuwa hawaogopi kitu, mzee Mwakyembe alikwenda pale wakamchomea!!!!!! kwamba madili yao yanalala!!!!! akatolewa ili waendelee kuiba vizuri, ngoja nisiongee mengi zaidi, please tunaomba waandishi wa habari waendelee kutuhabarisha hawa watu hatma yao ni nini, wataifishiwe vitu vyote, virudishe kodi yetu

    ReplyDelete
  14. Haya changanyeni miguu hiyo mkalipie hayo makontena wenyewe kabla hamjafuatwa huko mliko mtiwe pingu muaibike mitaani. Jipelekeni wenyewe Huyo nae alijisahau kama ni mfanyakazi wa serikali? Duh!!acha asimame kidogo aone utamu wa kukosa kazi kama watanzania wengine wenye maisha magumu. God bless you all viongozi wetu wapya na wachapa kazi.

    ReplyDelete
  15. Hili ni la kupongeza sana hapa hamna cha sisi wapinzani au sisi wenye chama. Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa Serikali isiyokusanya kodi ni Serikali Dhalimu. Mapato yanapotea kwa wafanyabiashara wakubwa wakati wadogo ndio wananyanyashwa kwa ushuru na kodi za kero kama za mazao na mifugo. Ni WAJIBU WA KILA MWANANCHI kulipa Kodi. Wakwepaji wakubwa wa kodi ndio wafadhili wakubwa wa chama ndio wanaotoa Tshirt na Kanga za chama kwa gharama ya kodi ya wananchi. Kwani huyu Mhindi hapa aliwahi kuchukuliwa hatua? na kama alichukuliwa hatua ni hatua ghani? https://www.youtube.com/watch?v=Xog6QcYb2bI angalieni hii video ya Mwigulu Nchemba. Sasa Wananchi wote tujenge tabia ya kudai risiti msipodai risit tunaibiwa na wafanya biashara. TRA tueni elimu ya kutosha kwenye hili tuachane na taifa ombaomba.

    Mheshimiwa Rais na Waziri Mkuu, sehemu nyingine za kuangalia ni hizi taasisi

    1. Mifuku ya Hifadhi ya Jamii- huko kuna ufisadi mkubwa sana hasa kwa wasimamizi wa miradi ya ujenzi. Wanajulikana kwa majina na wana utajiri mkubwa sana wachunguzwe wamepataje huo utajiri

    2. Mashirika ya Usimamizi kama TCRA, TPDC, etc huko kuna miungu watu nako Serikali inapoteza mapato mengi sana.

    3. Halmashauri - Huko wakurugenzi wanapiga sana sana hasa za miradi na mishahara hewa. Mapato hayakusanywi na ubunifu wa vyanzo vipya vya mapato hamna

    4. Mali Asili huko usiseme Mheshimiwa maana wapiga kampeni wako ndio shamba lao la kuvuna.

    5. Ardhi nako usiseme mheshimiwa nadhani hiki kiwe kipaumbele chako namba 2 na namba 3. Kila Halimashauri zipewe Target ya kupima maeneo kwa kila Mwaka walau kwa kipindi hiki cha uongozi wako wa miaka 10 maana najua utapita bila kupingwa 2020 walau nchi iwe imepimwa na mipango ya matumizi ya ardhi imefikia walau asilimia kubwa na hii itapunguza rushwa na migogoro na pia kuzipatia halmashauri mapato na kupunguza makazi holela holela.

    Kwa leo Waheshimiwa yangu ni hayo machache.

    Mwalimu Mkuu

    ReplyDelete
  16. Hongera sana JPM kwa kudhibiti mianya ya upotevu wa fedha za umma. Sehemu nyingine ni Bungeni. Wale wanaosaini kuwa wapo wakati hawapo Bungeni na kujichotea posho za bure.

    Wekeni mashine za alama za vidole kudhibiti unadhirifu wa posho Bungeni. Alipwe tu yule ambaye anafanya kazi za wananchi na wala siyo ujanja ujanja na wizi wa fedha za posho.

    ReplyDelete
  17. Ndugu michuzi naona tunahukumu haraka sana hasa kuhusu kusimamishwa kwa mkurugenzi mkuu wa TRA. Ama hakika nilidhani waziri mkuu alishatumia wadhifa wake kusimamisha wa husika. Lakini naona Mh Rais ameenda Mbali zaidi bila ya kumpa nafasi mkurugenzi mkuu kulifahamu hili jambo (maana yawezekana kabisa) akawa hakulifahamu maana nyaraka za TRA makontena hayo hayamo na nina imani anafanya kazi kwa kutumia systems na sio yeye kwenda physical pale kukagua kila kontena litokalo na ukipima haiwezekani kontena 300 kupotea kwa siku 27 za utawala wa Mh Magufuli. HilI linataka proper investigation laweza kuwa ni jambo la siku nyingi sana hata kabla Bade hajaanza kazi TRA maana na yeye sio wa siku nyingi hapo kwenye kazi.
    Hayo ndio maoni yangu.

    Nafurahia kasi ya uwajibishaji ningependa kuiona kwenye makampuni ya madini na migodini maana wakilipa kodi zinazostahili ama hakika budget ya mwaka unaofata hatuhitaji kuwa na msaada wa aina yoyote. Hao ndio muhimu zaidi kwa mustakabali wa kodi ya nchi hii. Wakilipa nadhani hata haya tuliyo yaona yatakuwa ni madogo sana.

    ReplyDelete
  18. Ahaa!!Kumbe ndivyo ilivyokuwa wanaiba hapo Bandarini!!Kusema kweli Niliwahi kutuma makonteina TZ, na yalipofika wakayaficha kwanza na baada ya wiki mbili kuyatafuta wakaniletea barua eti yamepotea.....
    Siamini kuwa ni hao tu waliosimamishwa,wao wengi.
    HIVYO BASI:
    1.LAZIMA WAPELEKWE MAHAKAMANI, WALIPE FIDIA ZA MAKONTEINA YA WATU YALIYOPOTEA.
    2.WALIPE PESA ZA KODI(importation tax) KWA SERIKALI.
    3.WALIO UZIWA MAKONTINA YOTE HAYO WATAFUTWE ILI NAO WAAJIBIKE.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...