Waandishi wa habari wa gazeti la Jambo Leo, wakifurahia kupata fagio walizokabidhiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Zahanati ya Mji Mwema Kigamboni, Dar es Salaam, Omary Kombe (kulia), katika hafla iliyofanyika katika chumba cha habari cha gazeti hilo, Dar es Salaam. 
Kombe ametoa msaada huo kuunga mkono maelekezo ya Rais Dk. John Magufuli ya kufuta sherehe za Sikukuu ya Uhuru ili wananchi washiriki siku hiyo kufanya usafi wa mazingira kwa lengo la kutokomeza ugonjwa wa kipindupindu nchini. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Katika kuunga mkono jitihada za rais Magufuli kuhisiana na swala zima la usafi wa mazingira, jumamosi hii (12/11/2016) tutakuwa tunafanya usafi eneo zima la Mji Mwema Beach. Eneo ambalo limekuwa sugu kwa uchafu wa mazingira, kwani kumekuwa na utupwaji holela wa taka hasahasa vifurushi. Tunawakaribisha wadau wote katika tukio hili muhimu litakaloshirikisha watu maarufu pia ambao wamejitolea kuunga mkono usafi huo. Chini ya balozi wa kujitolea katika kuhakikisha usafi wa mazingira unafanyika, Omary Komba.
    Mawasiliano 0659 740417

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...