Na Eleuteri Mangi-MAELEZO

Watumishi wameaswa kuzingatia taratibu za uhamisho na wametakiwa kuwa makini na utapeli pamoja na upotoshaji unaofanywa kupitia mitandao ya kijamii na matangazo mbalimbali yanayowataka  kulipia pesa ili kupata uhamisho.

Aidha, Serikali imewaonya watu wote wanaoghushi na kutumia vibaya nembo yake pamoja na mihuri kwa lengo la kuwalaghai wananchi na kujipatia fedha kwa njia isiyo halali.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari aliyoitoa leo jijini Dar es salaam, Msemaji wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Rebecca Kwandu amesema kuwa Serikali haitasita kuchukua hatua kali za kisheria kwa yeyote atakayepatikana na hatia ya kughushi nyaraka na kujipatia fedha kwa njia isiyo halali baada ya kuwarubuni wananchi.

Taarifa hiyo ya Serikali inafuatia kuzagaa kwa upotoshaji unasosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na matangazo yanayoeleza kuwa baada ya mtumishi kutuma maombi kwa Katibu Mkuu TAMISEMI na kukubaliwa, Katibu Mkuu atamtuma Afisa wake atakayepeleka majibu ya uhamisho na kumtaka mtumishi aliyeomba uhamisho kumgharimia  anapompelekea uhamisho jambo ambalo siyo kweli. 

Kwa mujibu wa TAMISEMI, miongoni mwa watu wanaosambaza taarifa za upotoshaji ni Charles Machali ambaye amejipachika cheo cha Afisa Mdhibiti Uhamisho na anapatikana kwa simu Na. ni 0782 803783 na 0674 583941 na barua pepe yake ni charles53gachari@gmail.com.

Baada ya taratibu za uhamisho kukamilika, Serikali hutangaza majina ya watumishi waliopata uhamisho kupitia tovuti ya Wizara  ambayo ni    www.tamisemi.go.tz

Taratibu za kawaida za uhamisho zinamtaka mtumishi kupitishia barua kwa kiongozi wake mahali anapofanya kazi na katika mkoa wake ambao ndio una jukumu la kuleta maombi hayo kwa Katibu Mkuu TAMISEMI.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...