THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.


There was an error in this gadget

Waziri Mkuu aitaka NHIF kuongeza bidii katika kutoa elimu ya Afya kwa Jamii

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipatiwa maelezo ya huduma zinazotolewa katika banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) na Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa Mfuko huo, Rehani Athumani, wakati alipotembelea Banda lao kwenye Maonyesho ya Nane nane, mkoani Lindi.
Waziri Mkuu akitoa maagizo kwa uongozi wa Mfuko wa kuongeza elimu hususan katika magonjwa ya unyanyapaa ndani ya jamii.
Mwanachama wa Mfuko akipata maelezo ya huduma zinazotolewa bandani hapo.


NCHI WAHISANI WATOA DOLA ZA MAREKANI MILIONI 802.15 KUKABILI MABADILIKO YA TABIA NCHI

IMG_1116
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akimkaribisha ofisini kwake Mwakilishi wa mtandao wa FANPRAN, Sithembile Ndema kwa ajili ya kusaini kitabu cha wageni kabla ya kuelekea kwenye ukumbi wa mikutano.(Picha na Zainul Mzige wa modewjiblog).

Na Mwandishi wetu
JUMLA ya dola za Marekani milioni 802.15 zimetolewa na nchi wahisani katika kusaidia mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi katika kipindi cha miaka miaka mine iliyopita.

Hayo yalielezwa na Mkurugenzi wa Kituo cha Mabadiliko ya tabia nchi Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) Profesa Pius Yanda wakati alipokuwa akitoa mada kuhusu utafiti alioufanya yeye na wenzake kuhusu mchango wa uwezeshaji mapambano hayo kutoka nchi marafiki.

Alisema kiasi hicho cha fedha ni sawa na wastani wa dola milioni 200 kila mwaka zilizokuwa zikipelekwa katika sekta mbalimbali nchini.

Alisema utafiti walioufanya ambao ulilenga kuona kiasi cha fedha zilizotoka kwa wafadhili kwa ajili ya miradi mbalimbali ni awamu ya pili ya utafiti ambao awali ulijikita kuona bajeti ya taifa inavyotumika kukabili mabadiliko ya tabia nchi.

Profesa Yanda ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere cha Mazingira amesema kwamba sehemu kubwa ya fedha ipo katika miradi ya maendeleo ambayo utekelezaji wake pamoja na kutosema kwamba unakabili mabadiliko ya tabia nchi, matokeo yake ndiyo yanayobainisha.
IMG_1128
Mkurugenzi wa Kituo cha Mabadiliko ya tabia nchi Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) Profesa Pius Yanda (kushoto) akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida (wa pili kushoto) huku wengine wakishuhudia zoezi hilo, Kulia ni Mwakilishi wa FANPRAN, Sithembile Ndema na wa pili kulia Mtafiti msaidizi kutoka ESRF, Ian Shanghvi.


TCRA YATOA ELIMU KWA WANANCHI KWENYE MAONESHO YA KILIMO ARUSHA

Gari maalumu la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) likiwa kwenye uwanja wa maonesho ya Nanenane Njiro jijini Arusha,wananchi wanaotembelea banda la TCRA hupata elimu namna gari hilo linavyofanya kazi. 

Mmoja wa wananchi akipata maelezo kwenye banda la TCRA kwenye uwanja wa Taso ,Njiro jijini Arusha.
Afisa wa TCRA,Oswald Octavian(kulia)akimweleza jambo namna taasisi hiyo inavyofanya kazi ya kusimamia mawasiliano nchini.


DK CYRIL CHAMI KUPEPERUSHA BENDERA YA CCM JIMBO LA MOSHI VIJIJINI


Video imepigwa na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.


Kutoka Maktaba: Magufuli - (2005) tutasafiri kutoka Mtwara hadi Bukoba kwenye barabara ya lami

WANANCHI wataweza kusafiri kutoka Mtwara hadi Bukoba kwenye barabara ya lami,hayo yalisemwa Bungeni Mjini Dodoma wakati Waziri wa Ujenzi John Magufuli alipokua akijibu swali la Martha Mlata (Viti Maalum-CCM), swali lililohoji juu ya ahadi ya Serikali katika kipindi cha awamu ya nne na ahadi hiyo iliyosema wananchi wataweza kusafiri kwa taxi toka Mtwara hadi Bukoba.

Waziri Magufuli alisema kuwa nia ya msemo huo ni kuonesha kwamba wananchi wataweza kusafiri toka Mtwara hadi Bukoba kwa lami na kuongeza kuwa lengo hilo limetekelezwa kwa mafaniko makubwa hadi kufikia asilimia 99 ya barabara yote kutokea Mtwara hadi Bukoba.

Hata hivyo ahadi ya Magufuli imetekelezwa kwa kuwa sasa barabara yote kuanzia Mtwara – Dar es Salaam- Dodoma-Singida- Nzega-Tinde-Usagara pamoja na Geita-Bwanga-Kyamyorwa hadi Bukoba yenye urefu wa kilometa zipatazo 1,989 imejengwa kwa kiwango cha lami.

Serikali ya awamu ya nne imetimiza ahadi ya wananchi ya kusafiri kwenye barabara ya lami kutoka Mtwara hadi Bukoba imetekelezwa kwa asilimia mia moja (100%).


NCHI WANACHAMA WAPITISHA TAMKO KUHUSU AGENDA MAPYA YA MAENDELEO ENDELEVU

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon, akiwa na Mabalozi Macharia Kamau wa Kenya na David Donoghue wa Ireland wakati walipozungumza na waandishi wa habari kuelezea namna mchakato wa majadiliano yaliyokamilisha na hatimaye kupitishwa nan chi wanachama Tamko kuhusu Ajenda za Maendeleo Endelevu baada ya 2015. Tamko hilo lilipitishwa jumapili usiku. Mabalozi wao ndio waliosimamia mchakato mzima wa majadiliano hayo.
Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi, muda mfupi baada ya kuahirishwa mkutano kwa mapunziko mafupi hapo siku ya ijumaa usiku na kisha mkutano kuendelea tena hadi alfajiri ya Jumamosi, wakarejea tena mchana na kuendelea tena hadi usiku wa kuamkia jumapili na kuendelea jumpily mchana hadi usiku walilopitisha tamko hilo. Pamoja na naye Mkurungenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestin Mushy.
Afisa Mkuu Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Bw.Songelael Shilla ambaye amekuwa akisimamia mchakato wa majadiliano yaliyopelekea kupatika kwa ajenda mpya za maendeleo endelevu baada ya 2015, aliyeketi nyuma ni Dk. Lorah Madete kutoka Tume ya Mipango hii ilikuwa ni Ijumaa usiku.

Baaada ya  majadiliano  makali yaliyodumu kwa wiki mbili  na wakati mwingine wajumbe  kulazimika kukesha hadi asubuhi. Hatimaye nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa,     Jumapili   usiku (Agosti mbili), wamepitisha kwa kauli moja,  rasimu ya  tamko kuhusu  Agenda ya  Malengo ya Maendeleo  Endelevu  2015.

 Katika kuhakikisha kwamba  ilikuwa ni lazima  tamko hilo likamilike na kupitishwa,  wajumbe walilazimika kukesha ndani ya  ukumbi wa mkutano  kulikokuwa kukifanyika  mkutano huo,  wakipimzika  kwa saa chache na kurejea tena na hatimaye kufanikisha kukamilishwa kwa raslimu hiyo siku ya jumapili majira ya usiku.

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiongozwa na  Mwakilishi wa Kudumu Balozi Tuvako  Manongi na Afisa Mkuu  Bw. Shilla,  kwa kushirikiana  na    wataalamu  kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,   wakiongozwa na Mkurugenzi wa  Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa,  Balozi Celestin Mushy,  Wataalamu kutoka  Tume ya  Rais Mipango,  Tanzania   Bara na Visiwani,   Wizara ya Fedha na  Asasi zisizo za Kiserikali,  imeshiriki kikamilifu katika  kipindi chote  miaka miwili  tangu kuanza kwa  mchakato wa majadiliano  hayo.

Tamko lilolopitishwa  i   Jumapili,   itawasilishwa mbele ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa katika  tarehe  itakayopangwa   kupitishwa   rasmi.

Viongozi Wakuu wa Nchi na  Serikali watapokea na  kupitisha tamko hilo katika mkutano wao   wa Kihistoria utakaofanyika mwezi  ujao (  25-27Septemba) hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.

Akionyesha kufurahishwa na kuridhika kwake baada ya  wajumbe  kupitisha tamko hilo  , Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, licha ya kuwapongeza wajumbe kwa kazi kubwa , kujituma kwao na zaidi kupitisha  rasimu hiyo kwa kauli moja,  amesema  anasubiri kwa hamu kuungana na Viongozi  Wakuu wa  Nchi na Serikali  zaidi ya 150 na  wawakilishi wengine katika mkutano  wa kilele utakaopitisha  za ajenda hizo za maendeleo endelevu kwa miaka 15 ijayo.

Akasema   mchakato mzima wa majadiliano ya maandalizi ya  tamko hilo ambao umedumu  kwa miaka miwili   umefanyika kwa   mshikamano,  weledi na ulikuwa shirikishi , ambapo hata makundi mbalimbali ya kijamii,  yalishiriki kwa ukamilifu.

Ban Ki  Moon, amesema,  ajenda mpya za maendeleo endelevu ambazo zinachukua nafasi ya  Malengo ya  Maendeleo ya Millenia  yanayofikia ukingoni mwaka huu, zinalenga katika kuwaondoa watu kutoka  katika  lindi la umaskini  pasipo kumwacha  yeyote.

“Napenda kuwapongeza nchi wanachama kwa uongozi wenu na kujituma kwenu, nawashukuru pia Mabalozi   Macharia Kamau  wa Kenya na   David Donoghue wa Ireland  kwa namna   walivyoendesha na kuusimamia mchakato huo bila  kuchoka na kwa kuonyesha  ufundi mkubwa  wa  kidiplomasia ” amesema Ban  Ki Moon.

 Na kuongeza kwamba Ajenda hiyo iitwayo: "kubadili dunia yetu: ajenda ya mwaka 2030 kwa maendeleo endelevu" inajumuisha masuala yanayowahusu wote ikilenga pia kuhakikisha Amani, ufanisi na kubuni ubia unaojali watu na sayari duni.


TAZAMA SHAMRA SHAMRA ZA MAGUFULI ALIVYOCHUKUA FOMU YA KUWANIA URAIS KWA TIKETI YA CHAMA CHA CCM


DIRA YA DUNIA YA IDHAA YA KISWAHILI YA BBC LONDON


JK AMWAGA WINO MISWADA MITANO YA SHERIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumanne, Agosti 4, 2015, ametia saini Miswada ya Sheria mitano hadharani ikiwa ni hatua yake ya mwisho kabisa kuridhia Miswada ya Sheria akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika sherehe iliyofanyika katika Ukumbi mpya wa Ikulu, Dar Es Salaam,Rais Kikwete ameridhia Muswada wa Sheria ya Mafuta na Gesiasilia, Muswada wa Uwazi na Uwajibikaji, Muswada wa Usimamizi wa Mapato ya Mafuta na Gesiasilia, Muswada wa Masoko ya Bidhaa na Muswada wa Tume ya Walimu.

Katika sherehe hizo zilizohudhuriwa na mamia ya wageni waalikwa, mawaziri wanaohusika na sekta hizo, Mheshimiwa George Simbachawene ambaye ni Waziri wa Nishati na Madini, Mheshimiwa Saada Mkuya ambaye ni Waziri wa Fedha na Mhe. Dkt. Shukuru Kawambwa ambaye ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi wametoa maelezo ya miswada hiyo mitano kabla haijaridhiwa na Rais Kikwete.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue pia wamehudhuria sherehe hizo ambazo vile vile zimehudhuriwa na mawaziri wa Serikali, mabalozi, wawakilishi wa taasisi zisizokuwa za Kiserikali (NGO’s)  na wadau wengine wa sekta ambazo Miswada yake imeridhiwa.

Hiyo ni mara ya pili kwa Rais Kikwete kuridhia Miswada ya Sheria hadharani. Mara ya kwanza ilikuwa mwaka 2009 wakati Rais Kikwete aliporidhia hadharani Muswada wa Sheria ya Matumizi ya Fedha katika Uchaguzi.

Aidha, hiio ni mara ya mwisho kwa Rais Kikwete kuridhia Miswada ya Sheria nchini kabla ya kuondoka madarakani mwanzoni mwa Novemba, 2015. Rais tayari amelivunja Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini hati ya Muswada wa Sheria ya Mafuta na Gesiasilia Jumanne, Agosti 4, 2015 katika Ukumbi mpya wa Ikulu, Dar Es Salaam akishuhudiwa na Waziri wa Nishati na Madini Mhe George Simbachawene na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Ngosi Mwihava.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini hati ya Muswada wa Usimamizi wa Mapato ya Mafuta na Gesiasilia Jumanne, Agosti 4, 2015 katika Ukumbi mpya wa Ikulu, Dar Es Salaam akishuhudiwa na Waziri wa Nishati na Madini Mhe George Simbachawene na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Ngosi Mwihava.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini kuridhia Muswada wa Usimamizi wa Mapato ya Mafuta na Gesiasilia Jumanne, Agosti 4, 2015 katika Ukumbi mpya wa Ikulu, Dar Es Salaam akishuhudiwa na Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya na Katibu Mkuu wizara hiyo Dkt. Servacius Likwelile.


STEVE NYERERE AZUNGUMZIA MCHAKATO WA KURA ZA MAONI ZA KUOMBA RIDHAA YA CCM KUWANIA UBUNGE KINONDONI


NAMNA YA KUPATA TIN NAMBA YA KAMPUNI,NGOs NA VIKUNDI/SACCOS

Na  Bashir  Yakub. 

Nilipoandika  kuhusu  namna  ya  kuunda kampuni  kwa  mujibu  wa  Sheria ya  Makampuni  sura ya 212 nilieleza  pia   kuwa   unapokuwa  umekamilisha  usajili  wa  kampuni     na  umepata  cheti  cha  usajili   yapo  mambo  mengine  ya  kufanya  kabla  ya  kuanza  rasmi  biashara. 

Moja  ya  mambo  hayo  nilisema   ukishapata  cheti unatakiwa  uende  manispaa  husika  ukapate  leseni  ya  biashara. Manispaa husika  ni  manispaa  ambako  ofisi  ya  kampuni  yako  itakuwa.  Kitu  kingine  baada ya  kupata  cheti  cha usajili  ni  kupata  namba  ya  mlipa  kodi (TIN). Ili  kampuni  ifanye  biashara  kisheria  inatakiwa  kuwa imepata  namba  hii.  

Yawezekana  wanahisa  kila  mmoja  anayo  namba  yake ya  mlipa  kodi   lakini  namba  hizo  haziwezi kutumika  kwakuwa  ni  za  watu  binafsi  na  si  za  kampuni.  Kampuni  inatakiwa  ipate namba  yake  inayojitegemea.  Halikadhalika  kwa  wanaoanzisha  vikundi kwa  mfano  saccos, na asasi  za  kiraia( NGOs) nao wanatakiwa  kuwa  na  namba  ya  mlipa kodi  ya  vikundi  hivyo. 

1.TIN  NAMBA  HUPATIKANA  WAPI.

Mamlaka  ya  mapato  Tanzania ( TRA) ndiyo  mamlaka  inayoshughulika  na  utoaji  wa  namba  za  mlipa  kodi. Awali  namba  hizi  zilikuwa  zikitolewa  makao  makuu  ya  mamlaka  ya  mapato ambapo  kwasasa  katika  kuboresha  huduma    wameweka  ofisi  za  kikanda  sehemu  mbalimbali  ambazo  huhudumia   wahitaji  wa  kanda  husika  kwa  mfano  kwa  Dar  es  salaam  eneo  la  ilala , buguruni, tabata, kariakoo  ofisi  zipo  makutano  ya  Shaurimoyo badala  ya  mnazi  mmoja  au  samora . Hata  hivyo   yapo  maeneo  mengine  ambayo  ofisi  za  kanda  hazijawekwa  kwa  mfano  mikoani  ambapo  wahitaji  hulazimika  kufuata  huduma  hii  makao  makuu  ya  mamlaka  ya  mapato.


TAARIFA KUTOKA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZIZitto Kabwe aongea na Viongozi wa Matawi ya jimbo la Urambo Mkoa wa Tabora wilaya ya Urambo

 Kiongozi Mkuu wa Chama cha ATC Wazalendo Zitto Kabwe akiongea na Viongozi wa Matawi ya jimbo la Urambo Mkoa wa Tabora wilaya ya Urambo katika Mkutano Mkuu wa Jimbo la Urambo.  (PICHA ZOTE  NA KHAMISI MUSSA)
 Wanachama wakimsikiliza kiongozi wao Mkuu.
 Wanachama wakimsikiliza Kionozi wao Mkuu kwa umakini mkubwa.
 Katibu Kata Urambo Kati, Mkulila Shabani akizungumza mbelea ya kiongozi Mkuu wa chama na Viongozi wa Matawi ya jimbo la Urambo Mkoa wa Tabora wilaya ya Urambo
 Mwenyeti Kata ya Kiloleni Tarafa ya  Usoke, Wilaya ya Urambo Kati, Juma Kamagi akizungumza mbelea ya kiongozi Mkuu wa chama na Viongozi wa Matawi ya jimbo la Urambo Mkoa wa Tabora wilaya ya Urambo.
Kiongozi Mkuu wa Chama cha ATC Wazalendo Zitto Kabwe akiongea na Viongozi wa Matawi ya jimbo hayo.


Bi. Bernadette Mathias akiimba Wimbo wa Tanzania Nakupenda kwa Kiswahili katika sherehe za kumtunuku JK shahada ya heshima chuo kikuu ya newcastle, australia

Bi. Bernadette Mathias ambaye kwa kushirikiana na mpiga piano mumewe Profesa Philip Mathias wakitumbuiza kwa wimbo wa "Tanzania, Tanzania nakupenda kwa moyo wote" kwa ufasaha na kusisimua waliohudhuria sherehe za Rais Jakaya Mrisho Kikwete kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Chuo Kikuu cha Newcastle nchini Australia Julai 29, 2015. 


MAGUFULI ACHUKUA FOMU KUWANIA URAIS TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI JIJINI DAR LEO,VIFIJO NA NDEREMO VYATAWALA

  
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt  John Pombe Magufuli na Mgombea Mwenza Ndugu Samia Suluhu Hassan wakionesha fomu zao za kuomba kugombea urais mara baada ya kuchukua kwenye ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi jijini Dar es salaam leo, ambapo walisindikizwa na viongozi mbalimbali pamoja na wanachama wa CCM na wananchi kwa ujumla wakiwa wamepanda kwenye gari maalum.
 Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dkt John Pombe Magufuli na Mgombea Mwenza Mhe Samia Suluhu Hassan wakionesha mkoba wenye fomu za Kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama hicho mbele ya wananchi  na wanachama wao nje ya ofisi ndogo ya CCM Mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam baada ya kutoka Tume ya Uchaguzi kuchukua Fomu za kugombea Urais  leo agosti 4, 2015.
  Mwenyekiti wa CCM Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwashukuru wananchi na Wanachama wa chama hicho walioshiriki shughuli nzima ya kumsindikiza Dkt John Pombe Magufuli ya kuchukua fomu ya kuwania kiti cha Urais kupitia chama hicho katika ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi jijini Dar leo.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana akiwashukuru Wananchi na wafuasi wa chama cha CCM walioshiriki shughuli nzima ya kumsindikiza Dkt John Pombe Magufuli ya kuchukua fomu ya kuwania kiti cha Urais kupitia chama hicho katika ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi jijini Dar leo.
 Mhe Samia Suluhu Hassan akiwashukuru Wananchi na Wanachama wa CCM waliojitokeza kwa wingi nje ya ofisi ndogo ya CCM Mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam baada ya kutoka Tume ya Uchaguzi kuchukua Fomu za kugombea Urais leo agosti 4, 2015.
Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dkt John Pombe Magufuli na Mgombea Mwenza Mhe Samia Suluhu Hassan nwakilakiwa na Mwenyekiti wa CCM Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wengine akipokewa katika ofisi ndogo ya CCM Mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam baada ya kutoka Tume ya Uchaguzi kuchukua Fomu za kugombea Urais leo agosti 4, 2015.
Picha ya pamoja
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akiwa sambamba na Katibu wa Itikadi na Uenezi  Taifa Nape Nnauye,Mwenyekiti wa CCM Mkoa Dar es Salaam,Ndugu Ramadhan Madabiba pamoja na pichani shoto Ndugu Januari Makamba aliyeshinda kura za maoni CCM jimbo la Bumbuli kwa pamoja wakimsindikiza Dkt Jonh Pombe Magufuli kuchukua fomu za kuwania Urais mapema leo jijini Dar. 
Wafuasi wa chama cha Mapinduzi wakiwa wamekusanyika nje ya Ofisi Ndogo ya Makao ya CCM mtaa Lumbumba wakishangwekwa wakati Mgombea Mteule wa Urais kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli aliyekuwa akienda kuchukua Fomu ya kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),jijini Dar leo. 
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA


Introducing Imperial Solutions for all your car needsWAKULIMA WATAKIWA KUFUATA USHAURI WA WATAALAMU NA KUFANYIA KAZI MAFUNZO WANAYOPEWA


 Afisa kilimo daraja la kwanza  wa halmashauri ya mbulu  Peter Sangawe   akiwa anaomuonyesha  Mkuu wa mkoa wa Manyara Dk Joel Bendera  jinsi ya kuifadhi  nafaka bila kutumia kemikali  .
Mkuu wa mkoa wa Manyara Dk Joel Bendera akiwa anakagua vitunguu vinavyolimwa na halimashauri ya mbulu.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI


TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LEO


BODI YA USAJILI WA WAHANDISI (ERB) YAKUZA AJIRA NCHINI

Msajili wa Bodi ya Wahandisi nchini Tanzania(ERB) Muhandisi Steven Mlope akiongea na waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam kuelezea mafanikio ya Bodi hiyo katika kipindi cha miaka 10 hasa ukuzaji wa sekta ya ajira nchini Tanzania.

NA.Aron Msigwa - MAELEZO.

Bodi ya Usajili wa Wahandisi nchini Tanzania (ERD) imefanikiwa kutengeneza ajira 1600 kwa Watanzania kufuatia usajili wa makampuni 160 ya ushauri wa kihandisi yaliyoanzishwa nchini kote nchini katika kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2005 hadi 2015.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuelezea mafanikio ya Bodi hiyo kwa kipindi cha miaka 10 Msajili wa Wahandisi nchini Tanzania (ERB) Muhandisi Steven Mlope amesema kuwa kwa kusajili makampuni 160 katika kipindi cha miaka 10 pia wamefanikiwa kusajili wahandisi wapatao 8496 ambao kwa ujumla wao wametengeneza ajira kwa Watanzania 256,480.


FAHAMU UHUSIANO ULIOPO KATI YA UNENE & UZITO ULIOZIDI (OBESITY & OVERWEIGHT ) NA TATIZO LA UKOSEFU/UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

Unene  na  uzito  uliozidi  ( Obesity )  ni  miongoni  mwa  vyanzo  na  visababishi  vikuu  vya  tatizo  la  ukosefu  na  upungufu  wa  nguvu  za  kiume.

Kwa   mujibu  wa  tafiti  mbalimbali  za  kitabibu, asilimia  kubwa  ya  wanaume  wenye   unene  na  uzito  uliozidi, wanakabiliwa  na  tatizo  la  ukosefu  na  upungufu  wa  nguvu  za  kiume.

KWANINI  WANAU
ME  WENYE  UNENE  NA  UZITO  ULIOZIDI  WANAKABILIWA  NA  HATARI  KUBWA  YA  KUPATWA  NA  TATIZO  LA  UKOSEFU  NA  UPUNGUFU  WA  NGUVU  ZA  KIUME.

Wanaume  wenye  uzito na  unene  uliozidi  wapo  katika  hatari  kuu  ya  kupatwa  na  tatizo  la  ukosefu  na  upungufu  wa  nguvu  za  kiume  kwa  sababu  kuna  uhusiano mkubwa  kati  ya  unene/uzito  uliozidi  pamoja  na  tatizo  la  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume.


BALOZI JOHN MICHAEL HAULE AWASILISHA HATI ZA UTAMBULISHO KWA RAIS WA JAMUHURI YA KENYA, LEO

Mheshimiwa Uhuru Kenyatta Rais wa Jamuhuri ya Kenya akimpongeza na kumkaribisha rasmi Mheshimiwa Balozi John Michael Haule mara baada ya kupokea Hati zake rasmi za utambulisho.
Mheshimiwa John Michael Haule, Balozi wa Tanzania nchini Kenya akiteta jambo na Mheshimiwa Rais Uhuru Kenyatta wa Jamuhuri ya Kenya mara baada ya kuwasilisha Hati za utambulisho.
Mheshimiwa Balozi John Michael Haule akiwa kwenye picha ya pamoja na Mabalozi wengine waliowasilisha Hati zao za utambulisho kwa Mheshimiwa Uhuru Kenyatta, Rais wa Jamhuri ya Kenya.
Mheshimiwa Balozi John Michael Haule akipokea shada la maua kutoka kwa Mke wake, Bibi Mary John Haule mara baada ya kuwasili kwenye makazi yake, Muthaiga 81 akitokea Ikulu ya Nairobi baada ya kuwasilisha Hati zake za utambulisho kwa Mheshimiwa Rais Uhuru Kenyatta.


MBENA KIDEDEA KURA ZA MAONI JIMBO LA MOROGORO KUSINI

Na John Nditi, Morogoro

WABUNGE wanne wa zamani katika majimbo ya mkoa wa Morogoro wamefanikiwa kutetea nafasi zao kwenye uchaguzi wa kura za maoni zilizofanyika Augosti 1, mwaka huu nchini kote kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).

Walionusurika kwa kutetea nafasi zao ni Mbunge wa Jimbo la Ulanga Mashariki, Celina Kombani, Ulanga Magharibi , Dk Haji Mponda, Jimbo la Morogoro Mjini Abdulaziz Abood na Jimbo la Gairo , Ahmed Shabiby .

Wabunge walioanguka katika kura za maoni ni pamoja na Innocent Kalongeries Jimbo la Morogoro Kusini aliyepigwa mwereka na Prosper Mbena, ambaye ni Katibu wa Rais Jakaya Kikwete, kwa kupata kura 9, 548, na Kalongeries akipata kura 7,714 na kushika nafasi ya pili, nafasi ya tatu imenyakuliwa na Zuberi Mfaume kwa kura 2,607.

Jimbo hilo lilikuwa wagombea sita akiwemo anayemaliza muda wake Augosti 20, mwaka huu , Kalogeries, ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro.

Mbali na hao wengine walikuwa ni Kessy Mkambala aliyapata kura 1,269 Lwitiko Beregu kura 740 , Zuberi Mfaume alijipatia kura 607, na Sudi Mpili alijipatia kura 347 .

Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki, Mgombea Omary Mgumba ameshinda kura za maoni kwa kupata kura 4,193, akifuatiwa na Jamila Mohammed Taji kura 3,497 wakati mbunge aliyekuwa akitetea nafasi yake Dk Lucy Nkya akiambulia kura 2,357, Jimbo hilo lilikuwa na wagombea 14.

Majimbo mengine ambayo wabunge watetezi wameshindwa kutetea nafasi zao ni pamoja na Mvomero, Mikumi, Kilombero, wakati jimbo la Kilosa lilikuwa wazi baada ya mbunge wake anaye maliza muda wake Mustafa Mkulo kung’atuka kwa hiari yake na kuwapisha wengine.
Prosper Mbena siku aliporejesha fomu ya kuomba kuteuliwa nafasi ya Ubunge , ( kulia) ni Katibu wa CCM Wilaya ya Morogoro Vijijiji, Shaibu Mtawa.
Mgombea wa Ubunge aliyeshinda kura za maoni Jimbo la Morogoro Kusini, Prosper Mbena ( wa kwanza kushoto) akiwa pamoja na mshindani wake, Kalongeries ( shati la kawaida).
Mbena ( kushoto) akisililiza maelezo ya mmoja wa wagombea mwezake.
Mbena akisaini daftari la orodha ya wagombea waliochukua na kurudisha fomu .


MAJAJI WA MAHAKAMA YA TANZANIA WAFUNDWA JUU YA USIKILIZAJI WA MASHAURI YA UCHAGUZI

Na Mary Gwera, Mahakama
JAJI Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman amewataka Majaji nchini kujiandaa na usikilizaji wa mashauri/kesi za uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

Hayo yalisemwa katika risala yake iliyosomwa na Mhe. Jaji Edward Rutakangwa, Jaji wa Mahakama ya Rufaa (T) kwa niaba ya Mhe. Jaji Mkuu, Mohamed Chande Othman alipokuwa akifungua rasmi Warsha ya siku mbili (2) ya Uhamasishaji wa Wahe. Majaji juu ya utatuzi wa migogoro ya Uchaguzi “Judges Sensitization Workshop on Electoral Dispute Resolution.” Katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Alisema kuwa warsha hiyo iliyoandaliwa na kudhaminiwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) inalenga katika kuwajengea uwezo Wahe. Majaji kukabiliana na kesi za uchaguzi na kusaidia Majaji kufanikisha kesi ziende kwa haraka/spidi na kwa haki.

“Warsha hii imekuja wakati muafaka ambapo nchi yetu ipo katika mchakato wa kuelekea uchaguzi mkuu ambao unatarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu, hivyo ametoa wito kwa Wahe. Majaji kujiandaa kushughulikia migogoro au mashauri ya uchaguzi,” Alisema Jaji Rutakangwa.

Alisema kuwa kwenye uchaguzi hapakosi malalamiko na kusema kuwa Mahakama imejiandaa kushughulikia mashauri yatakayoletwa Mahakamani kwa kasi na kwa haki.

“Sisi kama Mahakama tupo tayari kushughulikia mashauri yatakayoletwa Mahakamani kwa kasi na kwa haki, hivyo tunaiomba Serikali kutoa ushirikiano ikiwa ni pamoja na rasilimali fedha zitakazowezesha kumaliza mashauri hayo kwa wakati,” alisisitiza.

Kwa upande wake, Bw. Trasias Kagenzi, Mkurugenzi wa Wilaya ya Maswa ambaye pia ni Msimamizi wa Uchaguzi alisema kuwa Serikali imejiandaa vyema na mchakato mzima wa uchaguzi ambapo kwa sasa zoezi la uandikishaji linaendelea vyema.
“Tumejipanga vizuri katika mchakato mzima wa uchaguzi ikiwa ni pamoja na kuandaa usafiri, kuwa na wasimamizi wa uchaguzi wa kutosha, hivyo tuna imani kuwa zoezi hili litakwenda vizuri,” Alisema Kagenzi.

Warsha hiyo ya siku mbili iliyoanza tarehe. 03.08.2015 na kumalizika tarehe 04.08.2015 imekusanya jumla ya Majaji 46 wa Mahakama ya Rufaa na Mahakama Kuu, tayari warsha kama hiyo imeshafanyika kwa kundi lingine la Majaji waliokutana mkoani Arusha lengo likiwa ni kuwajengea uwezo katika usikilizaji wa mashauri ya uchaguzi.
Jaji wa Mahakama ya Rufani (T), Mhe. Jaji Edward Rutakangwa akifungua warsha ya Wahe. Majaji kwa niaba ya Mhe. Jaji Mkuu wa Tanzania, juu ya ushughulikiaji wa Mashauri ya uchaguzi uliofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Kundi la baadhi ya Wahe. Majaji na wageni wengine waalikwa wakiwa katika warsha hiyo.
Wahe. Majaji wakiwa katika warsha hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Warsha hiyo imedhaminiwa na UNDP.
 Washiriki wa warsha Wahe. Majaji wa Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu pamoja na Wadau wa UNDP wakiwa katika picha ya pamoja na meza kuu.


Zimebaki Siku Nane, Usikose Kongamano La kufungua Fursa