Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Balozi wa Korea nchini, Young-Hoon Kim, wakikata utepe kwa pamoja kuashiria uzinduzi rasmi wa Chuo kipya cha Ufundi Stadi cha VETA kilichojengwa Mkoa wa Lindi.Uzinduzi huo ulifanyika jana. Kulia ni Mkurugenzi wa VETA, Zebadia Moshi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,akibonyeza 'Alam', kuashiria uzinduzi rasmi wa Chuo kipya cha Ufundi Stadi cha VETA kilichojengwa Mkoa wa Lindi. Uzinduzi huo ulifanyika jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda mti wa kumbukumbu katika eneo la Chuo cha Ufundi Stadi cha VETA baada ya kuzindua rasmi chuo hicho kilichojengwa Mkoa wa Lindi. Uzinduzi huo ulifanyika jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,akiongozana na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Shukuru Kawambwa, Balozi wa Korea nchini, Young-Hoon Kim na Viongozi wa VETA, wakati akitembelea na kukagua baadhi ya majengo mapya yaliyojengwa ya Chuo cha Ufundi Stadi cha VETA, baada ya kuzindua rasmi chuo hicho mkoa wa Lindi jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Ghariub Bilal,akisikiliza maelezo kuhusu jinsi ya ufundishaji wanafunzi kwa kutumia mtambo wa kufua Umeme, kutoka kwa Mwalimu wa Umeme Veta, Majolo Mwigole, wakati Makamu alipofika kuzindua Chuo hicho cha VETA mkoa wa Lindi jana. Picha na Muhidin Sufiani-OMR.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. We thank the government for this progress. We need more of these VETA training centres. I hope this center will impart knowledge and skills to our people as well as promoting self employment.

    ReplyDelete
  2. Kheri,manake katika mikoa iliyokuwa nyuma kielimu ni huu ni mmojawapo.Tunategemea chuo kikuu pia kitajengwa muda si mrefu, chuo kikuuu cha serikali namaanisha.Manake tunahitaji huduma serikalini ambako ndiko tunakopeleka kodi na ndiko kwenye maslahi kwa watu wote

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...