Bwana Amini S. Mwanga wa Chuo Kikuu Dar es salaam anasikitika kutangaza kifo cha mdogo wake bwana Wilson Stephano Kidavi (pichani) kilichotokea tarehe 8 june 2012 huko Kibaha mkoa wa Pwani. Mwili wa marehemu umesafirishwa leo Juini 10, 2012 kwenda Ugweno, Kilimanjaro, kwa ajili ya mazishi yatakayo fanyika kesho Juma tatu tarehe Juni 11, 2012. Habari ziwafikie wana ukoo wote wa Mwanga, ndugu, jamaa, marafiki na wanafunzi walio soma na marehemu Kibaha Sc School na wafanya kazi wenzake, wana Kibaha pamoja na marafiki wa Kaka zake Dada zake pamoja na mashemeji wote
Bwana ametoa, Bwana ametwa
Jina lake lihimidiwe
AMEN














































Post a Comment